WAKATI zoezi la upigaji kura kwa waimbaji, mgeni rasmi na mikoa likiendelea, kundi la Ambassadors of Christ, ‘Kwetu Pazuri,’ limepigiwa kura na Watanzania  kwa ajili ya kushiriki kwenye Tamasha la Pasaka linalotarajia kuanza Aprili 20.

Kwa mujibu wa taarifa zilizotolewa na Makamu Mwenyekiti wa Tamasha la Pasaka, Abihudi Mang’era, kundi hilo limeanza kupigiwa kura siku chache zilizopita wakati baadhi ya waimbaji wa Tanzania wakiongoza katika zoezi hilo. Akizungumza na Pata Habari, Mang’era alisema kundi hilo linaendelea kupigiwa kura kwa wingi za uwepo wao katika tamasha hilo licha ya kuwa baadhi ya waimbaji wanaongoza kwa kuwa na kura nyingi.

“Tumewapa nafasi Watanzania wafanikishe taratibu za kupatikana kwa mgeni rasmi, mkoa  na waimbaji lakini tumeona wameanza kuchagua na waimbaji wengine kutoka nje na kura zao nyingi zimeangukia kundi la Ambasadors.” Alisema.

Mang’era alisema baada ya kuona hilo na kutaka kuwafurahisha watanzania, wanafikiria kufanya mazungumzo ya kundi hilo ili  kufanikisha mapendekezo ya wapiga kura. “Tunafikiria kufanya mazungumzo nao hivi karibuni, bila shaka kila kitu kitakwenda kama tulivyopanga kwa watanzania kupata kile wanachohitaji kwa maana ya Neno la Mungu kupitia kwa waimbaji watakaowachagua,” alisema Mang’era.

Aidha Mangera amewaomba na kuwakumbusha watanzania namna ya kuwapigia kura kwa waimbaji, mgeni rasmi na mikoa ambako ukitaka kumpigia mwimbaji andika neno pasaka acha nafasi kisha andika jina la mwimbaji unatuma kwenda namba 15327.

Pia kwa mgeni rasmi  andika neno pasaka acha nafasi kisha andika jina la mgeni rasmi unayetaka kumpigia kura tuma kwenda 15327, wakati mikoa unaandika pasaka acha nafasi jina la mkoa unaotaka kuupigia kura tuma kwenda namba 15327 piga kura uwezavyo ili upate mwimbaji na mgeni rasmi na mkoa unaopenda tamasha lifanyike.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Nyimbo zao ziko kwenye internet search nyimbo za DVD hii .. ni vema, amani moyoni, anayo heri, kuna siku, amani, huyo ni Yesu, kazi ya mikono yako, kazi tufanye. Kama wewe unapenda nyimbo za injili na usifurahie wewe basi tena.

    Mwaka 2011 kwaya hii ilipokuwa inatoka kutumbuiza Tanzania ilipata ajali Shinyanga vijana wao watatu akiwemo mmoja mtanzania aliyekuwa akiimba nao walipoteza maisha. Nyimbo zao za kiswahili zimeendelea kubariki wengi katika Afrika mashariki na kati.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...