Mkurugenzi Mkazi wa mradi wa Tuboreshe Chakula,Unaofadhiliwa na Shirika la misaada la watu wa marekani USAID,Bi. Rebecca Savoie katikati,akitoa paketi ya unga wa uji uliochanganywa na virutubishi kwa mmoja wa wakazi wa kata ya Mpunguzi aliyehudhuria uhamasishaji wa lishe kwenye kata hiyo.
Mkurugenzi Mkazi wa mradi wa Tuboreshe Chakula,Unaofadhiliwa na Shirika la misaada la watu wa marekani USAID Bi Rebecca Savoie katikati,na maofisa wenzake kutoka mradi huo wakifurahi na wananchi wa Mpunguzi kwa kupiga makofi wakati wa uzinduzi wa kampeni ya lishe kwenye kata hiyo leo.
Mkuu wa wilaya ya Dodoma mjini,Bwana Lephy Gembe akiwasili katika kata ya Mpunguzi katika shughuli za uhamasishaji wa kutumia vyakula vyenye virutubushi ambao unafanywa na USAID kupitia mradi wake wa Tuboreshe Chakula.
Mkurugenzi Mkaazi wa mradi wa Tuboreshe Chakula,Unaofadhiliwa na Shirika la misaada la watu wa marekani USAID Bi Rebecca Savoie katikati,akitoa hutuba kwa lugha ya Kiswahili katika sherehe za uhamasishaji juu ya faida na umuhimu wa Virutubishi kwa watoto,umri miezi 6-miaka 5.Sherehe hizo zilizofanyika kata ya mpunguzi wilaya ya Dodoma mjini..Kushoto ni Bwana Lephy Gembe aliyekuwa mgeni rasmi,na kulia ni Dr Generose mtaalamu wa lishe.
Mmoja wa wahamasishaji wa umuhimu na faida za virutubishi kwa watoto wenye umri wenye miezi 6 mpaka miaka 5,Tom David,akiwagawia uji uliopikwa ukaongezwa virutubishi,wamama wa kata ya mpunguzi,wenye watoto umri wa miezi 6-miaka 5.Ikiwa sehemu ya uhamasishaji na uelimishaji kwa vitendo.Kampeni hizi zinadhaminiwa na mradi wa USAID Tuboreshe chakula.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...