Mke wa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Mama Asha Bilal akiambatana na Mwenyeji wake,Shamim Mwasha wakati akikagua kazi mbalimbali za wanawake kwenye hafla ya Siku ya Wanawake,iliyofanyika jioni ya leo kwenye Ukumbi wa Diamond Jubilee,jijini Dar es Salaam..
Mke wa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Mama Asha Bilal na Mwenyeji wake,Shamim Mwasha wakipitia moja ya vitabu vya watoto vilivyotungwa na mmoja wa wanawake wa Tanzania.
Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya 8020 Fashions ambao ndio waratibu wa Hafla ya Siku ya Wanawake,Shamim Mwasha akizungumza machache kabla ya kumkaribisha mgeni Rasmi kuja kutoa hotuba yake.Hafla hiyo imefanyika jioni ya leo kwenye Ukumbi wa Diamond Jubilee,jijini Dar es Salaam.

Mgeni Rasmi katika Hafla ya siku ya Wanawake,Mke wa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Mama Asha Bilal akihutubia mamia ya kinamama waliohudhulia hafla hiyo.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...