Na Mwandishi Maalum 

 Uingereza imeeleza kuwa , mkutano wa kimataifa uliofanyika mwezi uliopitia jijini London, Uingereza na kujadili namna ya kukabiliana na biashara haramu ya wanyama pori duniani, haukulenga kumnyoshea kidole mtu yeyote.

Kauli hiyo imetolewa na Naibu Muwakilishi wa Kudumu wa Uingereza katika Umoja wa Mataifa, Balozi Peter Wilson wakati wa mkutano wa kundi la nchi marafiki kuhusu ujangili na biashara haramu ya wanyamapori.

Mkutano huo ulifanyika siku ya jumatano katika Uwakilishi wa Kudumu wa Ujeruman katika Umoja wa Mataifa, chini ya uenyekiti- weza wa Wawakilishi wa Kudumu wa Gabon na Ujeruman. Muwakilishi wa Kudumu wa Tanzania Balozi Tuvako Manongi alikuwa mmoja wa washiriki wa kundi hilo la nchi marafiki.

Mkutano huo ulikuwa na lengo la kubadilisha mawazo miongoni mwa marafiki wa nchi hizo ambazo zimefika 20. kuangalia ni kwa namna gani juhudi hizi za kukabiliana na ujangili na biashara haramu ya wanyama pori zinaweza kuungwa mkono ndani ya Umoja wa Mataifa lengo likiwa ni kuzipa juhudi hizi msukumo wa kisiaza pamoja na ushiriki mpana zaidi.

Naibu Muwakilishi Balozi Wilson aliombwa kutoa muhtasari wa matokeo ya mkutano huo wa kimataifa uliofanyika mwezi wa februari. Ambapo alianza kwa kusema, “ kwanza ningependa kulieleza hili, mkutano ule hakuwa wakunyosheana vidole, tuliuitisha kwa lengo la kujadiliana ni kwa namna gani tutashirikiana katika kuikabili biashara hii haramu ya wanyamapori pamoja na ujangili”.

Kwa ujumla Balozi Peter Wilson, aliwaambia wajumbe wa nchi hizo marafiki dhidi ya ujangili na biashara haramu ya wanyamapori kwamba mkutano ulikuwa wa mafanikio makubwa kuliko walivyokuwa wametarajia.

Akaeleza kuwa mwitikio wa ushiriki ulikuwa mkubwa sana, zaidi ya nchi 50 zilishiriki wakiwamo marais watatu, akiwamo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania pamoja na Mashirika ya Kimataifa.

Akasema kuwa mkutano huo ulitoka na tamko lenye nguvu ambalo linazungumzia mambo mengi yakiwamo uimarishiji na uboreshaji wa sheria na sheria za makosa ya jinai, uwezeshwaji wa jamii zinazoishi katika maeneo ya wanyamapori kama sehemu ya kuwawezesha kuwa na maendeleo endelevu.

Akaongeza kuwa tamko hilo pia linazungumza udhibiti wa hitajio na soko la pembe za tembo na raslimali nyingine zitokanazo na wanyamapori na akazitaka nchi nyingine ambazo hazikuhushuria mkutano huo kuunga mkono tamko hilo.

Akabainisha kwamba viongozi kutoka nchi za Afrika waliohudhuria mkutano huo, walionyesha ushirikiano mkubwa na pia wao wenyewe walitoka na mpngo mkakati wao wa kukabiliana na ujangili na biashara haramu ya wanayapori ikiwamo mikakati ya kuwalinda tembo Naibu Muwakilishi huyo wa Uingereza pia ameeleza kwamba viongozi wakuu wa serikali yake pamoja na Mwanamfalme wote wameonyesha utayari mkubwa katika kukabiliana na changamoto hii. Aidha nchi kadhaa zikiwamo Marekani, Canada na Jumuiya ya Ulaya zimetoa ahadi za kuchangia raslimali fedha kusaidia juhudi hizo.

Wazungumzaji wengine katika mkutano huo walikuwa ni watendaji kutoka CITES, UNODC na UNEP ambapo katika ujumla wao, walieleza kwamba ili juhudi za kuukabili ujangili na biashara haramu ya wanyapori ziweze kufanikiwa lazima pawepo juhudi na ushirikiano wa kimataifa.

Walieleza kwamba, ni kujidanganya kwamba nchi moja moja inaweza yenye peke yake kukabiliana na hatimaye kuumaliza ujangili na biashara haramu ya wanyamapori kutokana na ukweli kwamba, ujangili na biashara hiyo haramu mtandao wake ni mkubwa wenye sura ya uharifu wa kimataifa.

Baadhi ya wajumbe akiwamo Balozi Manongi, waliunga mkono umuhimu wa kundi hilo la marafiki kutakafari mbinu na mikakati ya kupata uungwaji mkono wa kisiasa kutoka ndani ya Umoja wa Mataifa. Na pia akasisitiza hoja ya udhibiti wa soko na hitajio la raslimali zitokanazo na wanyamapori.

Balozi Manongi akaeleza kwamba taasisi mbalimbali za kitaifa na kimataifa zimeonyesha utayari mkubwa wa kushiriki katika juhudi hizi za kuthibiti ujangili na biashara haramu ya wanyamapori na kwamba itakuwa vema kwamba utashi na utayari huu kutoka kwa wadau mbalimbali ukaenziwa na wahusika wote.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Duhh,!

    Mnyama Tembo ni mkubwa anatisha sana, lakini binadamu na udogo wake anatisha zaidi kwa kumuuwa tembo!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...