Katika hali isiyokuwa ya kawaida,Mashabiki wa timu ya Simba wameanza tena kung'oa viti vya kukalia uwanjani hapa na kuwatupia Mashabini wenzao wa Timu ya Yanga waliofurika kwa wingi uwanjani hapa,kwa kile kinachodaiwa kuwa hawataki kukaa nao sehemu moja.lakini kwa hali ilivyo hivi sasa Uwanjani hapa,ni dhahiri kabisa kuwa Mashabiki hao wa Yanga wanaweza kuujaza Uwanja huu hasa kwa jinsi wanavyozidi kuingia Uwanjani hapa.Uongozi wa Vilabu hivi viwili vikubwa hapa nchini unatakiwa kukaa chini na Mashabiki wao na kuwakanya kuhusiana na uharibifu wa Miundombinu wanaoufanya Mashabiki wao katika Uwanja huu wa Taifa,kwani kuendelea kwa vitendo hivi kunazorotesha sana soka letu.Picha zote na Othman Michuzi,Uwanja wa Taifa jijini Dar.

 Mashabiki wa Timu ya Simba wakiendelea kuwarushia viti Mashabiki wa timu ya Yanga kabla hata ya mtanange wenyewe kuanza uwanjani hapa.
 Viongozi wa timu ya Yanga wakiwaomba Mashabiki wao kuhama katika eneo hilo na kwenda kujibana katika eneo walilotengewa kama wana Yanga.  
 Mashabiki wa timu ya National Al Ahly wakiongea na Askari Polisi kuomba wakalizuie tatizo hilo.
 Askari Polisi wakiongea na Viongozi wa Timu ya Yanga ili waweze kwenda kuwaomba mashabiki wao waaondoke katika upande ule unaodaiwa kuwa ni wa Mashabiki wa Simba. 
 Mambo yalianza kama masihara huku wengine wakitaniana kabisa.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 8 mpaka sasa

  1. Aibu jamani viti vimewakosea nini. Dawa ya tatizo hili itafutwe kumaliza kabisa milele upuuzi huu na hasara inayofanywa.
    Huu si ushabiki ni ushenzi wa hali ya juu.

    MOTOLIVA

    ReplyDelete
  2. Kwani jamani kwa baadhi ya watu, utanzania/ uafrika ni defect? Uaribifu kama huu kweli? Pesa ngapi imetumika kutengeneza huo uwanja? Kama mtanzania badala ya kuutunza, kuuthamini, unangoa viti?
    Watu wengine hawana ustarabu. Hope wanachukuliwa hatua.

    ReplyDelete
  3. michuzi naomba usibanie hii comment

    huu ni upumbavu, ujanja ujanja na wizi wizi unaojengwa na kulindwa na TFF ndio husababisha yote haya, halafu watalaumiwa YANGA na SIMBA (don't get me wrong, i don't condone the behavior of these thugs)

    TATIZO ni kwa nini zaidi ya miaka mitano sasa tangu huu uwanja ufunguliwe bado watu wanaingia na kukaa kiholela ... viongozi wa TFF wengi washafika viwanja vya kisasa na kuona jinsi vinavyoendeshwa ... kila mtu analipia ticket yenye specific seat number, na kwa wenzetu uingereza wenye unazi wa soka kuliko sisi wametenga kabisa jukwaa dogo (5-10%) la away team, tickets zinauzwa kwa washabiki wa away team tu hilo eneo. Simba haikua home wala away team katika hii match, kwa nini police walikuwa wanawadekeza na huu utoto wao unaoiabisha nchi? tunaweza fungiwa tucheze matches bila washabiki kwa huu upumbavu!

    haya mawazo niliyatoa mwanzoni wa 2009 wakati TFF walipoomba maoni kuhusu uendeshaji wa uwanja wa taifa ... siwezi kujua kila kitu ila na uhakika haya ni mawazo chanya ndio maana wenzetu wanatumia utaratibu huu

    ReplyDelete
  4. The mdudu,huo upuuzi watu wanaufanya kutokana na serikali kua goi goi tunaomba serikali kuanzia leo huu uwanja usitumike kwa team yoyote ile hapa tanzania zaidi ya team ya TAIFA STARS hao wajinga wa simba na yanga wakajenge viwanja vyao mm binafsi I HATE THEM coz ni wajinga kuanzia viongozi wao mpaka wapenzi wao wote ni washenzi,,au kama vipi waziluhusu hizo team zingine but not SIMBA and YANGA,hii mitimu mm sizipendi na wala sitaki hata kuziona why nasema yote haya tena kwa uchungu,1 wajiulize hivi timu zao zimeanzishwa lini? Na why mpaka leo hii hawana cha kujivunia cha maana,,viwanja vya maana hawana,,2 timu zao kwenye mashindano makubwa wao kuchemsha tuu miaka nenda ludi,na mkome kutuvunjia viti vya uwanja wetu wa team ya TAIFA,

    ReplyDelete
  5. Haya yanatokea bongo tua. Pongezi unkel kwa kutuletea taswira za waharibifu hawa. Sasa hao polisi wanaodai nyongeza za mishahara wako wapi? au segerea imejaa. Hawa wamefanya uhaina wa kuharibu mali ya umma> athabu kali itolewe!!

    ReplyDelete
  6. Ushahidi upo unaonekana kwa nini Polisi hawakuwakamata, kazi yao ni nini uwanjani.Polisi wawajibike kwa hili

    ReplyDelete
  7. Hivi huu ushenzi wa wahuni kung'oa viti utaisha lini???

    SULUHISHO
    1) HIVI POLISI UWANJANI WANAJANYA NINI? WAWAKAMATE HAWA WANG'OA VITI NA KUWAPELEKA SEGEREA.
    2) POLISI WAWAJIBIKE KUSHINDWA KAZI YAO.
    3) KILA KITI KINA NAMBA. TIKETI ZIKATWE KWA NAMBA YA KITI. KILA KITI KITAKUWA NA MLINZI-MWENYE KITI CHAKE.
    4) HAWA WATU WANASURA GANI WASIOJUA KUWA NI HASARA KUFANYA UHARIBIFU KAMA HUU???
    5) UONGOZI WA UWANJA WATAFUTE MUAROBINI WA UGONJWA HUU SUGU-MAPEMA. KUNA SIKU WATA CHOMA UWANJA MOTO HAWA WANYAMA-MTU.

    ReplyDelete
  8. This comment has been removed by a blog administrator.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...