Hili ni eneo la Ubungo ambalo limekuwa na wimbi kubwa la
wafanya bishara wadogo wadogo kuegesha biashara zao za kila aina
pembezoni mwa njia za wapita kwa miguu jambo ambalo linasababisha
usumbufu mkubwa kwa watumiaji wa barabara hiyo.
Licha
ya usumbufu na kero hiyo, eneo hilo kutokana na msongamano wa watu
wengi sana, limekuwa ndio maskani kwa vibaka ambao hujipatia kipato chao
bila hata ya jasho kwa kujichanganya humo kama raia wa kawaida na
kufanya wizi.
Wakizungumza
watumiaji mbalimbali wa barabara hiyo wamelilalamikia Jiji na Manispaa
husika kwa kushindwa kuwataftia eneo husika wafanyabiashara hao wadogo
wadogo na kwamba kutokana na uzembe huo mkubwa wa kutowazuia nao
wameamua kuendelea kuleta kero
"Eneo
hili kwa kweli linatia Aibu sana kwa sababu hapa ndipo Lango kuu la
kuingia jijini na mara watu wanapo ingia wanakutana na kero hii ambayo
mimi binafsi naita ni uchafu, nasikitika sana kuona Jiji na Halmashari
husika wameshindwa kabisa kudhibiti na kuwataftia eneo husika hii ni
aibu"
Alizungumza mmoja wa watumiaji wa barabara hiyo ambaye hupita mara kwa mara.
Hii
ndiyo hali Halisi ya eneo kutoka Ubungo Darajani karibia na mitambo ya
Gesi hadi eneo la watu wanaopandia magari ya kwenda Mwenge? Je
Halmashauri ya Jiji hamlioni hili? Je Manispaa husikia nanyie hamlioni
hili? Au hili ni eneo halali limepitishwa kwa ajili ya kufanya biashara
hizi?
Hawa nao wanauza Viatu pande hizi kwa bei nafuu...
Wengine wanauza samaki katika eneo ambalo kiafya sio sahihi.
wanatafuta hela ya kula na kulipa pango ya chumba; ukiwafukuza wataenda wapi; wawe vibaka/majambazi?Afadhali ya hiyo kuliko kuwa kibaka au jambazi?Tunachoomba hali hiyo iondolewe sambamba na hao watu kuwahakikishia wanapata njia ya kuweza kuishi na familia zao na mahitaji mengine ya binadamu, shule, n.k.
ReplyDeleteKutafuta hela ya kula siyo sababu ya kuvunja sheria
ReplyDeleteMICHUZI NAOMBA USINIBANIE..
ReplyDeleteJambo hili linasikitisha sana. Viongozi wetu siku zote wanafanya ziara nchi za watu lakini hawajifunzi. Lakini siamini tatizo kama hili ni la kwenda kujifunza nje ya nchi. Viongozi lakini siku wanaimba vijana mjiajiri lakini hawatengenezi mazingira mazuri ya kujiajiri. Huu umekuwa kama wimbo. Hawa vijana mmeisha fahamu kuwa wanapenda sehemu zilizo karibu na vituo vya usafiri kama vituo vya mabasi. Sasa kwa nini Serikali isije na mkakati wa kuanza kutenga maeneo maalum karibu na vituo vya mabasi yaliyopimwa na kuandaliwa kwa ajili ya hawa vijana. Maeneo hayo yakitengwa na kuzungushiwa uzio vijana hawa watakwenda humo kwa sababu haitakuwa mbali na msongamano wa watu. Mnapoongelea kutengeneza maeneo mazuri ya uwekezaji ni kwa ajili ya wazungu tu? Tukiendeleza sera hizo daima tukiulizwa pamoja na kukua kwa uchumi kwa nini watu ni maskini jibu litakuwa hata mimi sijui. Tubadilike tukiona tatizo tusitafute simple solution. Tuanze sera hii ya kujenga maeneo ya biashara ndogondogo karibu na vituo vikubwa vya mabasi na tutafanikiwa kuwaondoa moja kwa moja kutoka barabarani.