Rais Jakaya Mrisho Kikwete akihutubia wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba mjini Dodoma leo
Makamu wa Rais Dkt Mohamed Ghalib Bilali, Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe Mohamed Chande Othman na Rais Mstaafu wa awamu ya pili Alhaj Ali Hassa Mwinyi na wajumbe wakifuatilia hotuba ya Rais Kikwete leo
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Shariff Hamad, Jaji Mkuu wa Zanzibar Mhe Makungu na Rais Mstaafu wa Zanzibar Mhe Amani Abeid Karume na wajumbe wakisikiliza hotuba ya Rais Kikwete leo
Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba Mhe Tundu Lissu akigonga meza kuashiria kukunwa na hotuba ya Rais Kikwete
Rais Kikwete akihutubia wajumbe wa Bunge Maalum
Rais Kikwete akisisitiza jambo katika hotuba yake
Waziri Mkuu Mhe Mizengo Pinda akifurahia jambo na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi, Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar Mhe Pandu Ameir Kificho, na Mhe Mohamed Seif Khatib na wajumbe wengine. PICHA NA IKULU
Ankali fanza juu chini utundike video clip nzima ya hotuba hii muhimu wengine macho yetu hayawezi kusoma kurasa zote za hotuba hii bila kuona kiza.
ReplyDeleteMdau
Raia Mkongwe
CCM mnaogopa nini serikali tatu? mbona kila siku mmo kwenye kuboresha tu miaka 50 inatosha kuboresha sayari nzima hili limeshindikana weka mfumo mpya msiogope.
ReplyDeletefanyeni mnavyotaka lakini ikija kwa wananchi ndio mtaona kura ya maoni inayotaka serikali tatu sasa sijui itabidi mrudi Dodoma kula posho mpya.
mdau.
Dodoma.
The mdudu,hongera mweheshimiwa rais kazi iliyobaki ni kwenu wajumbe kama alivyo sema rais serikali tatu inawezekana cha umuhimu ni kujipanga ni vipi hizi serikali zitajiendesha kimapato?,,mm kama the mdudu mchango wangu wa jinsi ya kujipanga na hizo serikali tatu ni jambo rahisi sn 1 tuige toka kwa wachina mtu au kiongozo yoyote yule akijihusisha na RUSHWA lazima anyongwe au maisha yake yote yaishie jela,2 mali zetu za nchi lazima ziwanufaishe wananchi wake,3 hakuna mgeni yeyote mwenye haki ya kumiliki ardhi ya nchi yetu,4 kuwe na msako wa wahamiaji haramu kila mwezi au kila siku,5 ukikamatwa au kujihusisha na madawa ya kulevya Maisha jela au kunyongwa,6 kubaka mwanamke au wanawake maisha jela au kunyongwa,7 kumuambukiza mtu au watu kwa makusudi na gonjwa la ukimwi Maisha jela au kunyongwa,8 ushoga marufuku mtu au watu ukikamatwa jela maisha au kunyongwa,hizi nguzo nane zikizingatiwa tu basi kila kitu mbele yetu kinaenda kiulaiiiini kabisa.nimesema hayo yote coz tunakila kitu so sioni sababu ya KUWA OMBA OMBA KWA MATAIFA YA NJE,asanteni wadau na kama kuna mtu anataka kunikosoa ajisikie free na kama ataungana na mm basi NGOMA INOGILE.
ReplyDeleteWow! utam wa hotuba hii inanikumbusha pale mwaka 1984 pale waziri mmoja wa Zanzibar alipomtania mchonga kwa kumwambia "moja na moja ni tatu".Lilikuwa ni wazo la utwashi wa kisiasa. Juliasi akakereka sana kwa utani huo.Kiongozi yule alidai serikali tatu mwaka 1984, lakini miaka 30 baadae zinanukia serikali tatu.Ama kweli utani utani mara huwa kweli.
ReplyDeleteMiongoni mwa waliokataa serikali tatu kipindi na kumchongea Jumbe hadi akafukuzwa kwenye nyadhifa zote za kisiasa alikuwa na Maalim Seif Hamadi ambaye leo ndie aliyebeba bendera za kuzidai serikali tatu, angalieni kuna nini hapa kama si siasa za kinafiki!! Brigedia Ramadhan Haji Faki akiwa Waziri Kiongozi ndiye aliyekejeliwa na Nyerere kwenye suala la 1 + 1 = 3, though mathematicians later proved that it could be possible for ! + 1 to produce the said results!!
ReplyDeleteVipi Ziwa Nyasa tunalo kalia Kikao Msumbiji kwa Chissano tunalo ama tumesha nyang'anywa?
ReplyDeleteNaona kimya tumeahidiwa Kikao kinakaa juzi na jana adi leo bado bila bila!!!
huyu mtikila mimi huwa kuna vitu sikubaliani nae , lakini hapa kwenye huu muungano kasema kweli kuwa una watu ambao wana manufaa nao , nakubaliana na mtikila kuwa turudishiwe tanganyika yetu , muungano hatuna haja nao , hivyo visiwa havina lolote la maana, kama petroli na sisi ipo tena na gesi juu achilia mbali dhahabu na almasi tulizonazo , hatuhitaji kabisa hivi vidudu vidogo dogo vinavyojiita vizanzibari , tuna uwezo wa kuendelea vizuri sana tukiwa peke yetu , tutawapa ushirikiano kama majirani na ndugu kwa kuwa tumeshachanganya damu , lakini mara hii na sisi tunataka tanganyika yetu yenye bendera yake kamili na kila kitu
ReplyDeleteSeif anataka Mamlaka Kamili ya Zanzibar (MKZ) na sio serikali tatu. Kama lazima kuwe na Muungano, bac tuwe na Muungano wa Mkataba kama vile EU. Yaani tunakubaliana kupashana habari juu ya hali za hewa, jua kali au upepo kwa ajili ya vyombo vya baharini! Lakini Zanzibar iwe nchi kamili.
ReplyDeleteBroo mdau! sasa hizo ni siasa za kinafiki au huyo uliemtaja ndio mnafiki?
ReplyDeleteMimi niko uk nielewesheni tanganyika na zanzibar ziliungana ikazaliwa tanzania sasa vipi bado zanzibar bado ipo na tanganyika sikuijua kumbe ilshaungana na zanzibar sasa jibu ni moja tanzania
ReplyDeleteHuu sio muungano wa juice kwamba labda ukishakuchanganya huwezi kuchanganua huu ni mchangano (mixture) sasa inawezekana kila mmoja ajue cha kwake....
ReplyDelete