Bondia iddi bonge akiwa ulingoni
Refarii Pembe Ndava akiwapatia maelezo mabondia Idd Bonge na Bernard Mwakasanga kabla ya mpambano wao uliofanyika Manzese
Bondia Iddi Bonge kushoto akimtwika Bernard Mwakasanga ngumi wakati wa mpambano wao uliofanyika manzese Dar es salaam Bonge alishinda kwa k,o ya raundi ya kwanza katika mpambanio huo Picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com

Bondia Iddi Kipandu .Iddi Bonge' mwishoni mwa wiki iliyopita alikata ngebe za Bernard Mwakasanga 'Shoka ya Bucha; baada ya kumtwanga kwa K,O ya raundi ya kwanza katika mpambano wao wa uzito wa juu uliofanyika Manzese Dar es salaam

mpambano huo uliokuwa na mashabiki wengi wa kike na kiume ulivuta hisia za watu mbalimbali ambapo baadhi ya mashabiki walikuwa wakisema hapa K,O tu ata hivyo mashabiki wengi walikuwa upande wa Bonge ambao walikuja kumshangilia na ngoma pamoja na filimbi

Bonge alipiga ngumi ya kwanza na kumfanya 'Shoka ya Bucha ' kwenda chini kama pakacha alipo hesabiwa na kusimama aijapita mda akapigwa ngumi nyingine na kudondoka kama mnazi hapo hapo refarii pembe ndava akakatiza mpambano na kumpatia ushindi bonge akimwacha mwakasanga anagalagala kwa ngumi nzito ngumi ya kushiba ya uzito wa juu

mara baada ya mpambano huo bondia Iddi Bonge alijigamba kwa sasa ana mpinzani ila anasikia tu jina la bondia Alphonce Mchumiatumbo ambapo amemtahadhalisha ole wake akutane na mikono ya mwanaume mchumiatumbo anacheza na wachovu ndio mana anawakaslisha mapema tu raundi ya kwanza na ya pili mimi nikikutana nae nitakuwa sina msalie mtume nae nitahakikisha namsambalatisha raundi za awari tu

katika mpambano huo uliosindikizwa na mabondia mbalimbali ambapo bondia Salum Kombe alimpiga kwa pointi Ally Jagalaga uku Amani Bariki ' Manny Chuga' akimsambaratisha kwa TKO ya raundi ya nne Selemani Motto na Kassimu Gamboo akimpiga bila huruma bondia  Mohamed Babeshi kwa K,O ya raundi ya tatu na Ally Ramadhani akitoa droo na Ashrafu Selemani katika mpambano wea uzito wa juu bondia halidi manjee alishindwa kufurukuta kwa Shabani Mtengera baada ya kupigwa kwa point na Hassani Mandula alimtwanga Ally Bugingo kwa point wakati Fadhili Majia akimpiga bila huruma Juma Selemani kwa K,O ya raundi ya nne

Mchezo huo wa masumbwi uliokuwa ukisimamiwa na chama cha ngumi za kulipwa nchini PST chini ya Emanuel Mlundwa
 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 7 mpaka sasa

  1. Kwa muonekano ktk picha, inaelekea Mwakasanga alipigwa kabla ya pambano kuanza!!

    ReplyDelete
  2. Mbona ana kiriba tumbo (kitambi)!

    ReplyDelete
  3. Health and Safety regulations hakuna katika tasnia ya boxing Tanzania?

    Maana mabonia hawa wawili hawajakidhi dhana 'usalama kazini' labda wachunia tumbo kama kina Don King wanataka kutengeneza pesa bila kujali madhara ya kifo, kilema cha kudumu n.k kwa mabondia wasiokuwa katika hali nzuri ya kimchezo kama hawa.

    Mdau
    Diaspora

    ReplyDelete
  4. Ndio mara ya kwana naona bondia mwenye kitambi cha saiz hii. Yaani ukipigana nae itabidi lazima ushindwe kwa sababu utadhani unapambana na Kangaroo mwenye mtoto. Unakwepa ngumi moja kumbe kuna ngumi nyingine inakuja kutoka kwenye kifuko !!

    ReplyDelete
    Replies
    1. Umenivunja mbavu kiongozi.

      Delete
  5. hii sio yenyewe uzito si lazima upimwe kwanza? Huyu bonge na kitambi chote hicho hawezi kuwa daraja moja na huyu mpinzani wake.

    ReplyDelete
  6. h ahahahahaa! Duuh hii ya leo kali. Yaani hapa nimecheka kweli na hawa mabondia.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...