Bondia iddi bonge akiwa ulingoni
Refarii Pembe Ndava akiwapatia maelezo mabondia Idd Bonge na Bernard Mwakasanga kabla ya mpambano wao uliofanyika Manzese
Bondia Iddi Bonge kushoto akimtwika Bernard Mwakasanga ngumi wakati wa mpambano wao uliofanyika manzese Dar es salaam Bonge alishinda kwa k,o ya raundi ya kwanza katika mpambanio huo Picha na www.superdboxingcoach. blogspot.com
Bondia Iddi Kipandu .Iddi Bonge' mwishoni mwa wiki iliyopita alikata ngebe za Bernard Mwakasanga 'Shoka ya Bucha; baada ya kumtwanga kwa K,O ya raundi ya kwanza katika mpambano wao wa uzito wa juu uliofanyika Manzese Dar es salaam
mpambano huo uliokuwa na mashabiki wengi wa kike na kiume ulivuta hisia za watu mbalimbali ambapo baadhi ya mashabiki walikuwa wakisema hapa K,O tu ata hivyo mashabiki wengi walikuwa upande wa Bonge ambao walikuja kumshangilia na ngoma pamoja na filimbi
Bonge alipiga ngumi ya kwanza na kumfanya 'Shoka ya Bucha ' kwenda chini kama pakacha alipo hesabiwa na kusimama aijapita mda akapigwa ngumi nyingine na kudondoka kama mnazi hapo hapo refarii pembe ndava akakatiza mpambano na kumpatia ushindi bonge akimwacha mwakasanga anagalagala kwa ngumi nzito ngumi ya kushiba ya uzito wa juu
mara baada ya mpambano huo bondia Iddi Bonge alijigamba kwa sasa ana mpinzani ila anasikia tu jina la bondia Alphonce Mchumiatumbo ambapo amemtahadhalisha ole wake akutane na mikono ya mwanaume mchumiatumbo anacheza na wachovu ndio mana anawakaslisha mapema tu raundi ya kwanza na ya pili mimi nikikutana nae nitakuwa sina msalie mtume nae nitahakikisha namsambalatisha raundi za awari tu
katika mpambano huo uliosindikizwa na mabondia mbalimbali ambapo bondia Salum Kombe alimpiga kwa pointi Ally Jagalaga uku Amani Bariki ' Manny Chuga' akimsambaratisha kwa TKO ya raundi ya nne Selemani Motto na Kassimu Gamboo akimpiga bila huruma bondia Mohamed Babeshi kwa K,O ya raundi ya tatu na Ally Ramadhani akitoa droo na Ashrafu Selemani katika mpambano wea uzito wa juu bondia halidi manjee alishindwa kufurukuta kwa Shabani Mtengera baada ya kupigwa kwa point na Hassani Mandula alimtwanga Ally Bugingo kwa point wakati Fadhili Majia akimpiga bila huruma Juma Selemani kwa K,O ya raundi ya nne
Mchezo huo wa masumbwi uliokuwa ukisimamiwa na chama cha ngumi za kulipwa nchini PST chini ya Emanuel Mlundwa
Kwa muonekano ktk picha, inaelekea Mwakasanga alipigwa kabla ya pambano kuanza!!
ReplyDeleteMbona ana kiriba tumbo (kitambi)!
ReplyDeleteHealth and Safety regulations hakuna katika tasnia ya boxing Tanzania?
ReplyDeleteMaana mabonia hawa wawili hawajakidhi dhana 'usalama kazini' labda wachunia tumbo kama kina Don King wanataka kutengeneza pesa bila kujali madhara ya kifo, kilema cha kudumu n.k kwa mabondia wasiokuwa katika hali nzuri ya kimchezo kama hawa.
Mdau
Diaspora
Ndio mara ya kwana naona bondia mwenye kitambi cha saiz hii. Yaani ukipigana nae itabidi lazima ushindwe kwa sababu utadhani unapambana na Kangaroo mwenye mtoto. Unakwepa ngumi moja kumbe kuna ngumi nyingine inakuja kutoka kwenye kifuko !!
ReplyDeleteUmenivunja mbavu kiongozi.
Deletehii sio yenyewe uzito si lazima upimwe kwanza? Huyu bonge na kitambi chote hicho hawezi kuwa daraja moja na huyu mpinzani wake.
ReplyDeleteh ahahahahaa! Duuh hii ya leo kali. Yaani hapa nimecheka kweli na hawa mabondia.
ReplyDelete