Moja kati ya studio ambayo inafanya vizuri katika utayarishaji wa muziki jijini dar es salaam sinza lego Flexible music imekuja tena na Mfalme wa Rhymes Afande Sele na ngoma yake mpya inayoitwa Mwendo kasi aliyoifanya katika studio hizo. 
 Mwendo kasi ni ngoma ambayo inaelezea ajali mbali mbali zinazotokea barabarani ambazo zinasababishwa na uzembe wa madereva na kusababisha vifo vya wananchi, akiwa amewashrikisha wasanii kutoka mkoani Morogoro Dyna Nyange na Bullet. 
 Pia wimbo huo ambao umetengenezwa na mtayarishaji kutoka Flexible Music anayeitwa Mbatizaji akiwa ameutengeneza kwa kiwango cha hali ya juu kutokana na vyombo na ubora wa studio.
 Kwa mashabiki wa Afande Sele mkae tayari kwa kile kitu ambacho amekizungumza katika wimbo huo maana amezungumza mengi kama unavyojua Mfalme wa Rhymes huwa akitoa kitu hakosei kwa mashabiki wake. 
 Katika wimbo huo amewazungumzia kwa wale madereva ambao wanakunywa pombe kisha wanaingia barabarani kumata uskani na kuendesha gari kwa mwendo wa kasi na kusababisha ajali pia ameongea kuhusu abiria ambao wanakaa kimya wakati dereva akiwa anaendesha gari kwa kasi. 
 Na Pia kwa madereva ambao wanaongea na simu huku wanaendesha magari, pia ku overtake katika kona kali maana nao wanaweza kusababisha ajali na kupoteza uhai wa binadamu maana uhai hauji mara mbili.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...