Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Rais Jakaya Kikwete amefanya Ziara ya siku moja katika Vikosi vya Jeshi la Wanannchi wa Tanzania (JWTZ) vya Komando na Uhandisi Medali vilivyopo Mkoani Morogoro.

Akizungumza katika kikao maalum na Maafisa pamoja na Askari wa vikosi hivyo,Rais Kikwete amesema ameridhishwa sana na utimamu wa vikosi hivyo kimafunzo na pia amehidi kukiongezea vifaa zaidi kikosi cha Uhandisi wa Medani ili kiweze kupambana na majanga hapa nchini.

Rais Kikwete pia amelitaka Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) kubuni mikakati ya kuondokana na Makazi ya muda.

Katika Kikao hicho,Rais Kikwete aliligusia swala ta tatizo la Maji linalovikabili vikosi hivyo,ambapo ameahidi kulishungulikia ndani ya kipindi hiki cha mwaka 2014.

Katika ziara hiyo,Rais aliambatana pia na Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mhe. Joel Bendera, Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue, Wakuu wa Kamandi, Wakuu wa Matawi Makao Makuu ya Jeshi, Makamishna Wizarani na Wajumbe wa Mabaraza ya Ulinzi na Usalama wa Wilaya na Mkoa wa Morogoro.
Amiri Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akiwasili kwenye Kikosi cha Komando kuanza ziara yake ya kujionea hali na utimamu wa vikosi vya JWTZ Mkoani Morogoro.
Amiri Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akipewa maelezo kwa kutumia mchoro kuonesha mzunguko mzima wa maeneo atakayotembelea katika kikosi cha Komando.
Amiri Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akiangalia kupitia kilengeo maalum kinachotumiwa kwenye silaha na makomando kulengea shabaha.

BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 5 mpaka sasa

  1. we are going to be an economic super power,therefore we need a powerful army,and we have it.Godbless JWTZ AND TANZANIA.

    ReplyDelete
  2. The mdudu,mm nalipenda sn jeshi letu la wananchi wa Tanzania yaani JWTZ.pongezi sn kwa ukakamavu wenu hakika mkofiti sn.

    ReplyDelete
  3. NAOMBA SUALA LA VIFAA VYA ULINZI TUSIFANYE MASIHARA. MIYE HAYA HAPA:
    (1) ANGA YETU IWE SALAMA KUTOKANA NA UVAMIZI WOWOTE ULE. NAOMBA KAMA TUTAKUWA NA UWEZO WA KUPATA ANGALAU S380 KWA IDADI INAYOSTAHIKI TULIANGALIE HILO. TUTUMIE VYUO VYETU KUTAFITI NJIA ILIYO YA JUU ZAIDI KULINDA ANGA. TUSIWAMINI SANA MAREKANI N.K., HAWACHELEWI KUTUGEUKA
    (2) ANTI-MISSILES. CHINA KUNA KAMPUNI YAO IPO, WANAWEZA KUSAIDIA ILO. TENA KWA DOLA KAMA BILIONI TANO HIVI. NA WANAWEZA SAIDIA TECHNOLOGY TRANSFER PIA. UTURUKI WAMESHAINGIA NAO MKATABA. DEFENSE SYSTEM YAKE INAFANANA NA ILE YA NATO AU YA WEZA KUWA ZAIDI.
    (3) NJIA ZA MAWASILIANO TUJITEGEMEE; HASAHASA KWA AJILI YA KUONGOZA MAKOMBORA, NDEGE ZA KIVITA, N.K.
    (4) TUHAKIKISHE TUNATENGENEZA NDEGE ZA KIVITA WENYEWE
    (5) TUFANYE TAFITI NA VIFAA VINGINE. SHUKRANI.

    ReplyDelete
  4. ehee nyie wabongo mnapiga kelele kuhusu raisi ajey. ndiyo huyo hapo pembeni aliyevaa nguo za blue sina haja ya kumtaja picha inajitosheleza. mark this space!

    ReplyDelete
  5. To mdau number 1,This is a good prophecy, I believe it is going to be fulfilled. Believe or not Tanzania is going to be an economic super power. May everybody out there pray for this country so that we can have a very suitable constitution.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...