Na Josephat Lukaza wa Lukaza Blog
Nimelazimika Kuandika Ujumbe huu kwaajili ya kuutarifu umma wa watanzania mara baada ya kupokea Ujumbe mfupi wa Sms kutoka Kwa rafiki yangu Mroki Mroki juu ya Kuingiliwa kwa akaunti ya Facebook na kuandika Ujumbe wa Kitapeli.

Huu ni Ujumbe ulioandikwa katika Ukurasa wa Rafiki yangu Mroki Mroki katika Ukurasa wake wa Facebook ukijaribu Kuwaaminisha watanzania Juu ya Mikopo inayotolewa na Kutumia Mbinu mbalimbali ili kuweza kutapeli watu.

Baada ya kuona Ujumbe Huo Mroki Mroki aliamua kuwajulisha Baadhi ya Rafiki zake kuweza kumsaidia Kuwataarifu wengine kuhusu ujumbe kuwa Siyo Mroki Mroki aliyeandika Ujumbe huo bali ni Matapeli wa Mtandaoni walioweza kuingilia akaunti yake ya facebook na kuweza kuandika Ujumbe huo wakijaribu kuwaaminisha Umma kama wanatoa Mikopo Bila Riba.
Napenda Kuchukua Nafasi hii Kuwataarifu watanzania kuwa HUU NI UTAPELI MSITHUBUTU KUTUMA PESA MTAIBIWA.
USHAURI WANGU KWA WATUMIAJI WA MITANDAO HII PAMOJA NA BARUA PEPE.

Tuwe na Utaratibu wa Kubadilisha mara kwa mara Namba au Maneno ya Siri tunayotumia katika Kuingilia katika akaunti zetu za barua pepe au akaunti zetu za facebook .Kwa kufanya Hivi tunaweza kuzuia watu kuingilia Akaunti zetu Kwa kiasi kikubwa .

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...