Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akimjulia hali mtangazaji wa kituo cha Televisheni cha Channel Ten na Magic Radio FM mpiganaji Salum Mkambala aliyelazwa katika Taasisi ya Mifupa ya MOI leo katika Hospitali ya Taifa muhimbili anakotibiwa majeraha baada ya kuapata ajali na kujeruhiwa vibaya wiki iliyopita Picha na Freddy Maro
Home
Unlabelled
JK amjulia hali mpiganaji Salum Mkambala wa channel ten leo
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Huyu rais bwana, Mungu ambariki sana. Huwezi ukawa binadamu mkamilifu kwa kila kitu, watasema hivi au vile ambavo wangependa uwatendee wananchi. Lakini huwezi kumridhisha kila mmoja. Katika awamu zote 4 za uongozi wa juu wa taifa letu, kwa huruma ya kweli toka moyoni kama binadamu binafsi na si kama rais, J.Kikwete namba 1 kwakweli. Huko ni kuguswa kiubinadamu. Angejali nafasi yake angekaa tu ikulu. Angekuwa anagombea awamu nyingine tungesema kampeni ili aonekane mwema, lakini alishaingia ya mwisho. God bless by president Kikwete. Kama raia nina haki ya kutoa maoni nionavyo na si lazima nifikirie sawa na wengine. Najua utamaduni wetu wengi umekuwa tu kwenye ukosoaji hasi kwa kila jambo....
ReplyDeleteMdau,
USA
Mbona ujihisi mdau ni maoni mazuri jiamini. Hongera Jk
DeleteNakubaliana na maoni ya mdau wa mwanzo kabisa hapo juu na kuyaunga mkono 100%. I wish kungelikuwa na uwezekano, basi angestahili kutunukiwa miaka mingine mitano ya uongozi (Raisi) akaendelea kuongoza, ikawa kama ni tuzo ya pekee ya shukran, upendo na heshima. Mbali ya wadhifa wake kikazi, hata ki ubinaadam tu ni dhahiri wema, upendo, huruma na heshima kwa rika zote, bila kujali tofauti zao, hiyo ni silka yake, haijalishi ati kwa kuwa kiongozi, la khasha! Ubinaadam ni khulka yake. Mwenyeez Mungu mlinde na muongoze kila palipo pema na penye kheri, mzidishie uadilifu, imani na upendo kwa nchi na raia wake. Bless you our President JK.
ReplyDeleteKwa kweli hata mimi naungana na wadau waliotoa maoni hapo Juu anastahili Pongezi kubwa ni mfano wa kuigwa na Mungu ambariki kwa hilo amjalie Afya njema.....
ReplyDeleteInshaalah m.Mungu atamjaalia yote mema.
ReplyDeleteBhuba.