Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akimjulia hali mtangazaji wa kituo cha Televisheni cha Channel Ten na Magic Radio FM mpiganaji Salum Mkambala aliyelazwa katika Taasisi ya Mifupa ya MOI leo katika Hospitali ya Taifa muhimbili anakotibiwa majeraha baada ya kuapata ajali na kujeruhiwa vibaya wiki iliyopita Picha na Freddy Maro

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 5 mpaka sasa

  1. Huyu rais bwana, Mungu ambariki sana. Huwezi ukawa binadamu mkamilifu kwa kila kitu, watasema hivi au vile ambavo wangependa uwatendee wananchi. Lakini huwezi kumridhisha kila mmoja. Katika awamu zote 4 za uongozi wa juu wa taifa letu, kwa huruma ya kweli toka moyoni kama binadamu binafsi na si kama rais, J.Kikwete namba 1 kwakweli. Huko ni kuguswa kiubinadamu. Angejali nafasi yake angekaa tu ikulu. Angekuwa anagombea awamu nyingine tungesema kampeni ili aonekane mwema, lakini alishaingia ya mwisho. God bless by president Kikwete. Kama raia nina haki ya kutoa maoni nionavyo na si lazima nifikirie sawa na wengine. Najua utamaduni wetu wengi umekuwa tu kwenye ukosoaji hasi kwa kila jambo....
    Mdau,
    USA

    ReplyDelete
    Replies
    1. Mbona ujihisi mdau ni maoni mazuri jiamini. Hongera Jk

      Delete
  2. Nakubaliana na maoni ya mdau wa mwanzo kabisa hapo juu na kuyaunga mkono 100%. I wish kungelikuwa na uwezekano, basi angestahili kutunukiwa miaka mingine mitano ya uongozi (Raisi) akaendelea kuongoza, ikawa kama ni tuzo ya pekee ya shukran, upendo na heshima. Mbali ya wadhifa wake kikazi, hata ki ubinaadam tu ni dhahiri wema, upendo, huruma na heshima kwa rika zote, bila kujali tofauti zao, hiyo ni silka yake, haijalishi ati kwa kuwa kiongozi, la khasha! Ubinaadam ni khulka yake. Mwenyeez Mungu mlinde na muongoze kila palipo pema na penye kheri, mzidishie uadilifu, imani na upendo kwa nchi na raia wake. Bless you our President JK.

    ReplyDelete
  3. Kwa kweli hata mimi naungana na wadau waliotoa maoni hapo Juu anastahili Pongezi kubwa ni mfano wa kuigwa na Mungu ambariki kwa hilo amjalie Afya njema.....

    ReplyDelete
  4. Inshaalah m.Mungu atamjaalia yote mema.
    Bhuba.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...