Mtalii kutoka nchini Ujerumani anayefahamika kama Bi. Jeanne Traska (32) akiwa na muongoza wageni Athuman Juma leo majira ya saa mbili na nusu asubui wamekwama katika kilele cha Mawenzi Mlimani Kilimanjaro kwa kamba iliyonasa na kuwafanya wasiweze kushuka chini wala kwenda juu.
Bi. Jeanne na Athuman Juma walianza kupanda mlima kupitia Kampuni ya Nordic Tours tarehe 18.3.2014 kwa kutumia njia ya Rongai - Kibo –Marangu safari ambayo ingewachukua siku tano. 
Hadi sasa taarifa za awali zinaonyesha kuwa Bi. Jeanne alitakiwa kwenda kileleni Kibo lakini katika mazingira yasiyofahamika alibadili uamuzi na kuelekea kilele cha Mawenzi ambacho huwa hakitumiwi na watalii isipokuwa kwa kujaza fomu maalum inayoonyesha kuwa mgeni amekubali kwa hiyari yake kupanda kilele hicho.
Shirika la Hifadhi za Taifa kwa kushirikiana na Kampuni ya Nordic Tours wanaendelea na jitihada za uokoaji kwa kutumia askari ambao wanaelekea eneo la tukio pamoja na helikopta itakayosaidia zoezi la uokoaji kwa kutegemea na hali ya hewa itakavyotulia ambapo hivi sasa kuna mawingu mazito katika eneo la mlima.
Umma utaendelea kufahamishwa maendeleo ya jitihada za uokoaji kadri zitakavyopatikana.

Imetolewa na Idara ya Mawasiliano
Hifadhi za Taifa Tanzania

22.03.2014

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. Watu wengine vichwa vigumu tu. Yeye kajaza form za kupanda Kibo alafu kwa mawazo yake mwenyewe kaamua kuelekea mawenzi. Sasa anatuingizia hasara kwa gharama za Helkopta na Jeshi letu kuacha shughuli zao kwenda kumtafuta. Tunaomwombea apatikane kwa haraka na mzima wa afya ili aweze kutueleza ni sababu gani zilizomfana aelekee huko.

    ReplyDelete
  2. Hivi vijamaa kaidi sana na ifanyike namna ya kumpatia fundisho yeye na wengine, nyambaff

    ReplyDelete
  3. Kilichomfanya abadili uelekeo ilikuwa ni nini au amekuwa naye ni ndege ya Malaysia kubadili uelekeo? ndo ajifunze kwenda alikoelekezwa sio anakotaka yeye

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...