Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Kijiji cha Wangama, Fred Mgata (kulia) akikabidhi kadi za chyama hicho kwa Katibu wa CCM Mkoa wa Iringa, Hassan Mtenga baada ya yeye na wanachama wengine 50 wa Chadema kuamua kukihama na kujiunga CCM katika mkutano wa kampeni za CCM uliofanyika  katika Kijiji hicho kilichopo Kata ya Luhota, Iringa Vijijini leo. Mgombea ubunge wa Jimbo la Kalenga kupitia Chadema ambaye ni mzaliwa wa kijiji hicho,  Grace Tendega alikuwa chini ya uongozi wa Mgata.
 Mgata akisalimiana na mgombea wa CCM Jimbo la Kalenga, Godfrey Mgimwa
 Mgata akipongezwa na wafuasi wa CCM kwa kitendo chake cha kuamua kuihama Chadema na kujiunga na CCM
 Katibu Mkuu wa CCM Mkoa wa Mtwara, Shaibu Akwilombe akihutubia katika mkutano wa kampeni katika Kijiji cha Wangama.
 Ofisa wa Umoja wa Vijana wa CCM Makao Makuu, Mariana Shonzaakimuombea kura  mgombea ubunge wa CCM, Mgimwa.

 Mgombea ubunge Jimbo la Kalenga kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Godfrey Mgimwa 9kulia) akilakiwa kwa shangwe na vigeregere na wananchi wa Kijiji cha Ikuvilo, Kata ya Luhota alipowasili kwa ajili ya mkutano wa kampeni za uchaguzi mdogo wa jimbo hilo leo Iringa Vijijini.PICHA ZAIDI BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...