Kwa siku za hivi karibuni matokeo ya mitihani yamekuwa sio mazuri sana na kuna baadhi ya watu wengi wanalaumu mitandao ya kijamii na internet kwa hili, kwamba inawafanya wanafunzi wawe busy kufanya mambo yasiyo ya msingi na kusahau kusoma.
Kwa kiasi Fulani ni kweli kwani kumekuwa na ongezeko la idadi ya vijana nchini Tanzania wanaojiunga na mitandao ya kijamii na internet kwa ujumla. Hata hivyo, ongezeko hili sio jambo la kuliangalia kwa jicho baya bali kulikumbatia kwani linaweza kusaidia wanafunzi wa sekondari, hasa sasa hivi ambapo kuna website kwa ajili ya wanafunzi wote Tanzania kukutana na kujadiliana masomo na topic mbali mbali wanazofundishwa darasani, na masuala yote ya kielimu kwa ujumla. Website hiyo inaitwa myElimu.com.
Given Edward, mwanzilishi wa myElimu Project, amesema website hiyo itawasaidia wanafunzi kujadiliana na wanafunzi wenzao mambo mbali mbali ya darasani, popote pale walipo. MyElimu.com itamuwezesha mwanafunzi wa shule yoyote ile, mfano ya Dar-es-Salaam, kujadiliana na wanafunzi wengine wa mkoa wowote wa Tanzania mfano mwanza, Arusha au Mbeya kuhusu masomo yao ya darasani.
Hii ina maana kwamba mwanafunzi aliyeko shule ya sekondari Kibasila, anaweza kuanzisha mjadala na wanafunzi wenzake wa Azania, Shaaban Robert, Nyakato au St. Francis wakaweza kujadiliana naye ndani ya mtandao huo wa myElimu.com. Safi!
MyElimu.com inapatikana kwa lugha 32 duniani nah ii itawezesha hata watembeleaji wa mtandao huo kutoka nje ambao hawajui Kiswahili na kiingereza waweze kutoa michango yao ambayo inaweza kutafsiriwa kuja kwa tena kuwa kwa Kiswahili au kiingereza kutegemea na chaguo la mtu.
Kitu kizuri kuhusu myElimu.com ni kwamba kuna sehemu ya games ambapo members wake wanaweza kwenda na kucheza pale ambacho watakuwa wameboreka au kuchoka kwenye discussions au wakiwa wanasubiri kitu kwenye mijadala yao..
Given aliitangaza rasmi myElimu siku 3 zilizopita katika post iliyosomeka:-
"I've been working on an initiative. Creating a platform where students all over Tanzania can meet and discuss school topics and every academic related issue. Currently it's difficult for students to share information mainly due to geographical distances. Nevertheless, with the increase in books with no single authorized source, it has been hard for students to know what materials are correct and good for use, hence they're stuck with wrong things.
So I created My Elimu. My Elimu is a project which will make it possible for students in Dar es Salaam to exchange ideas and learn together with students in Arusha, Mwanza, Iringa and all other parts of Tanzania through www.MyELimu.com. It will be a meeting point for all students from Form 1 to Form 6 to meet and help each other out.
When you visit the website, you will be met with an interactive user interface that displays forums of various subjects of which you will select any that interests you and start or join a topic discussion. You need to register to the website in order to participate or start a discussion. Guests can only read the discussions but not participate."
Kwa wanafunzi wote wa sekondari Tanzania kuanzia form 1 mpaka form 6 mnashauriwa mjisajli kwani ni sehemu nzuri ya kuweza kujikuza kielimu na kutumia internet kwa manufaa yako. Unaweza kujisajili moja kwa moja hapa http://goo.gl/2NvPbO au kwa kutembelea http://goo.gl/ j1kMzh na kisha kubonyeza “Register”. Ukijisajili ndio utaweza kuanzisha mijadala na kushiriki katika mijadla iliyoanzishwa tayari.
Big up Given!! Labda waziri wa elimu atakuunga mkono kuona namna ya kuiboresha ili ifikie kiwango ulichokusudia na pia kutoa vitabu na miongozo toka wizari. Tanzania ina kila kitu, na kila vipaji. Tunahitaji uongozi bora tu ili tuendelee.
ReplyDeleteMdau Canada
Given Edward, Hongera saaana kwa Uenezi huu na Ahsante sana kwa Ukombozi wa Elimu yetu Tanzania!
ReplyDeleteHuu Mpango umeuleta wakati mwaka kabisa wakati hali ya kiwango chetu cha Elimu kikiwa kimeshuka vibaya sana na kuanguka kwa Mitihani kuliko kithiri kwa Ubaya wa Matokeo ya Mitihani.
Tunaomba wananchi tuchangie kuuwezesha Mfumo aliouleta Given uweze kuwafikia wanafunzi kwa wingi na kwa ujazo mpana zaidi mfano:
1.ULE MPANGO WA LAPTOP KWA WANAFUNZI UINGIZIWE MFUMO HUU ILI WAWEZE KUSOMEA KWA KUTUMIA LUPUTOPU.
2.MITAALA ZAIDI IINGIE NDANI YA MFUMO HUU TENA IKIBIDI MITAALA IREKEBISHWE NA KUKIDH MAHITAJI NA WAKATI TULIO NAO. (Ukweli ni kuwa Elimu tuliyo nayo ni ya mwaka 1978 wakati ule wa TES (Tanzania Elimu Supplies) na Shirika la Elimu Kibaha wakati tukiwa ktk zama za DOT.COM hivyo ndiyo maana wimbi hili la mabadiliko ya Tekinolojia limeweza kuwazamsha wanafunzi wakafeli masomo kwa kutumia Mitandao ya Jamii vibaya huku Mfumo wa Elimu ukiwa haija rekebishwa na kwenda na wakati tulio nao.
3.Pia NECTA (Baraza la Mitihani la Taifa) na WIZARA YA ELIMU NA MAFUNZO YAUFUNDI wanahitajika kulitumia Jukwaa hili ili kuwezesha Mitihani ya Taifa kufikishwa kwa njia za KIDIJITALI kwa Watahiniwa badala ya Makabrasha kitu ambacho kinawezesha Mitihani kuvuja kwa urahisi na kuanguka kwa Kiwango cha Elimu hapa nchini Tanzania.