Timu ya Manchester City imeibuka na Ubingwa wa kombe la Capital One baada ya kuifunza mpira timu ya Sunderland kwa kuichabanga magoli 3-1 katika mchezo wa fainali uliochezwa uwanja wa Wembley,Machi 2,2014.


Katika mchezo huo uliokuwa ni mkali na wa kuvutia,Timu ya Sunderland ndio iliyokuwa ya kwanza kuona lango la Manchester City mnamo dakika ya 10 ya mchezo kupitia kwa Mchezaji wake,Fabio Borini katika kipindi cha kwanza.


Kipindi cha pili kilianza kwa kasi na Timu ya Manchester City haikufanya ajizi katika hilo na kuamua kuimiminia mvua ya magoli timu ya Sunderland kupitia kwa wachezaji wake Yaya Toure,Samir Nasri na Jesus Navas na kuipatia timu yao hiyo Ubingwa wa Kombe la Capital One.
Wachezaji wa Timu ya Manchester City wakishangilia Ubingwa huo wa Kombe la Capital One.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...