Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akizungumza na Wajasiliamali-VICOBA mbalimbali katika mkutano uliofanyika mapema leo asubuhi  ndani ya ukumbi wa Kata ya 15,katika Wilaya ya Temeke.Kinana aliwapongeza VICOBA hao kwa kuchapa kazi nzuri na kuwa waaminifu katika mazingira yao ya kufanya kazi.Aidha amewataka akina mama na vijana mbalimbali kutobweteka na badala yake wajitume kufanya kazi,katika suala zima la kujipatia maendeleo yao sambamba na kujikwamua na Umaskini.Ndugu Kinana amefanya ziara yake leo ya siku moja ndani ya Wilaya ya Temeke,ikiwa na lengo la Kuimarisha Uhai wa Chama hicho,kukagua miradi mmbalimbali  na kuhamasisha utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya mwaka 2010.
 Mbunge wa Jimbo la Temeke,Abbas Mtemvu akielezea namna alivyoweza kuwakutanisha watu wa kada mbalimbali katika kuunda VICOBA kwa ajili ya Maendeleo yao,katika Wilaya ya Temeke mapema leo wakati wa mkutano uliofanyika ndani ya ukumbi wa Kata ya 15,Mbele ya Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Abdulrahman Kinana alipokutana na VICOBA hao alipokuwa kwenye ziara yake ya siku moja wilayani humo.
 Baadhi ya akina mama mbalimbali waliojiunga kwenye VICOBA wakishangilia jambo,wakati wa mkutano mfupi uliowakutanisha na Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana,ambaye alizungumza nao na kuwatia moyo katika juhudi zao mbalimbali za kupambana na kujikwamua na lindi la umaskini.Kinana aliwaasa VICOBA hao kutobweteka na badala yake wafanye kazi kwa bidii na kujitegemea bila ya kusubiri ajira.
 Meneja Mradi wa kiwanda cha kuzalisha gesi kilichopo kata ya Mtoni,Bwa.Richard Matari akifafanua jambo mbele ya Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana alipotembelea mradi huo na kujionea hali halisi ya eneo hilo.
 Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akipata maelezo ya mradi huo wa kuzalisha gesi na changamoto zake,Kiwanda hicho mpaka sasa hakifanyi kazi kutokanana kukumbwa na changamoto mbali mbali na kupelekea kusimama kutofanya kazi mpaka sasa. 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...