Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete
akiwa katika picha ya pamoja na mgeni wake, Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje wa
Ujerumani muda mfupi kabla ya kufanya mazungumzo ya faragha (tete-a-tete ) huko
Ikulu tarehe 25.03.2014.
Rais Dkt.
Jakaya Mrisho Kikwete na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa
Mheshimiwa Bernard Membe wakipiga picha
ya pamoja na Waziri wa Mambo ya Nje wa Ujerumani Mheshimiwa Dkt. Frank-Walter
Steinmeier na ujumbe aliofuatana nao wakati wakipomtembelea Rais Dkt. Kikwete
huko Ikulu tarehe 25.3.2014.
Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete na ujumbe wake wakifanya mazungumzo na
Waziri wa Mambo ya Nje wa Ujerumani, Mheshimiwa Dkt. Frank-Walter Steinmeier na
baadhi ya viongozi aliofuatana nao wakati
walipomtembelea Rais Dkt. Kikwete huko Ikulu tarehe 25.3.2014.
Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akiwaonyesha wageni wake jengo la ikulu
sehemu iliyojengwa na Wajerumani (jengo halionekani pichani) mara baada ya
kufanya mazungumzo na ugeni huo.
Rais Dkt.
Jakaya Mrisho Kikwete akifuatana na mgeni wake Waziri wa Mambo ya Nje wa
Ujerumani Dkt. Frank- Walter Steinmeier wakitoka nje kwenda kuona sehemu ya
jengo la ikulu lililojengwa na Wajerumani wakati wakiitawala Tanganyika. Wengine
waliofuatana nao ni Balozi wa Tanzania huko Ujerumani Mheshimiwa Phillip Marmon
na Mkurugenzi wa Idara ya Ulaya na
Marekani katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Ndugu Dorah
Msechu.
Rais
Dkt. Jakaya Kikwete akimkaribisha Ikulu kwa mazungumzo Waziri wa Mambo ya Nje wa Ujerumani
Mheshimiwa Dkt. Frank-Walter Steinmeier. Waziri huyo aliwasili nchini tarehe
25.3.2014 kwa ziara ya kikazi ya siku moja.PICHA NA JOHN LUKUWI.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...