Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akihutubia Wananchi wakati wa kufunga Kampeni za Uchaguzi wa jimbo la Kalenga jioni ya leo,katika kijiji cha Kidamali,kata ya Nzihi Iringa vijijini.
Mkutano wa kufunga kampeni ukiendelea kwenye kijiji cha Kidamali kata ya Nzihi jioni ya leo.
Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akimnadi Mgombea Ubunge wa Jimbo la Kalenga kwa tiketi ya chama hicho,Ndugu Godfery Mgimwa,wakati wa mkutano wa kufunga kampeni katika jimbo la Kalenga,katika kijiji cha Kidamali kata ya Nzihi,Iringa Vijijini mkoani Iringa.Uchaguzi wa jimbo la Kalenga unafanyika kesho siku ya jumapili,Machi 16,kuziba pengo la aliyekuwa Mbunge wa jimbo hilo,Waziri wa Fedha na Uchumi,Marehemu Dk.William Mgimwa.
Mgombea Ubunge jimbo la Kalenga (CCM),Godfrey Mgimwa akimtambulisha mke wake,Bi.Robby Mgimwa kwa wananchi wa kijiji cha Kidamali kata ya Nzihi,ambako kumefanyika mkutano wa kumfunga kampeni jioni ya leo.
Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akizungumza jambo na Mhadhiri wa chuo kikuu cha Tumaini na Mtangazaji wa Radio One na ITV,Godfrey Gondwe.
Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana na Mgombea Ubunge jimbo la Kalenga (CCM),Ndugu Mgimwa wakiwapungia mikono wananchi jioni ya leo kwenye mkutano wa kufunga kampeni za chama hicho.
Mgombea Ubunge jimbo la Kalenga (CCM),Ndugu Mgimwa akiwa amebebwa juu juu na Wafuasi wa chama hicho,mara baada ya kuwasili kwenye Mkutano wa kufunga kampeni za cha hicho,zilizofanyika katika kijiji cha Kidamali,Kata ya Nzihi,Iringa vijijini.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...