Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Seif Rashid wakati akitoa tamko kuhusu ugonjwa wa kifua kikuu kwenye ukumbi wa wizara hiyo mjini Dodoma leo.
Baadhi ya waandishi wa habari wakimsilikiza Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Seif Rashid wakati akitoa tamko kuhusu ugonjwa wa kifua kikuu kwenye ukumbi wa wizara hiyo mjini Dodoma leo
Meneja Mpango wa kudhibiti kifua kikuu na ukoma, Dk. Beatrice Mutayoba wa kwanza kulia , katikati ni Naibu Meneja wa mpango huo, kushoto ni Afisa wa mpango huo Dk.Deus Kamara wote kutoka Dodoma.Picha na Magreth Kinabo -Maelezo
======== ====== =======
Na Magreth Kinabo-
Imeelezwa kuwa ugonjwa wa kifua kikuu ni ugonjwa wa tatu ambao unasababisha vifo vya watu wengi hapa nchini baada ya Malaria na Ukimwi.
Kauli hiyo imetolewa leo na Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Seif Rashid wakati akitoa tamko kuhusu ugonjwa huo kwenye ukumbi wa wizara hiyo mjini Dodoma, ambayo itaandhimishwa Machi 24, mwaka 2014 hapa nchini na nchi nyingine duniani .
Aidha kwa mujibu wa takwimu za Wizara hiyo zinaonesha kuwa idadi ya wagonjwa wa ugonjwa huo imeongezeka kutoka 11,000 mwaka 1980 hadi kufikia 63,892 mwaka 2012. “ Utafiti unaonesha kuwa zaidi ya asilimia 30 ya vifo vya watu vya watu walioathirika na ukimwi vinatokana na kiifua kikuu.
“Tangu kuzuka kwa ukimwi hapa nchini ,inakadriwa kuwa asilimia10 ya waathirika wa ukimwi wana ugonjwa wa kifua kikuu na takribani asilimia 40 ya wagonjwa wa kifua kikuu wana maambukizo ya VVU. Hali hii inafanya kifua kikuu kuwa miongoni mwa changamoto kubwa katika mapambano dhidi ya ukimwi na katika vita vya kutokomeza umasikini hapa nchini,” alisema Dk. Rashid.
Dk. Rashid aliongeza kuwa miongoni mwa sababu nyingine zinazochangia kuongezeka kwa idadi ni msongamano wa watu mijini, makazi duni ya watu na wagonjwa kuchelewa kupata matibabu.Aliitaja kauli mbiu ya mwaka huu “ Fikia kila mtu Gundua .Tibu na Ponya mgonjwa wa TB” .
Aliongeza kuwa sasa takribani zaidi ya watu milioni mbili hufariki kwa ugonjwa huo kila mwaka na asilimia kubwa ya vifo hivyo hutokwa Barani Afrika hususa Kusini mwa Jangwa la Sahara. Hivyo Tanzania ni nchi ya 14 kati ya nchi 22 zenye idadi kubwa ya wagonjwa wa ugonjwa huo duniani.
Alisema miongoni mwa mikoa inayoongoza kuwa na wagonjwa wapya wengi kwa takwimu za mwaka 2012 kati ya mikoa iliyoathirika kwa tatizo hilo ni Dares Salaam 13,983,Mwanza 5,946 na Shinyanga 4,074.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...