Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Abdulrahman Kinana pichani kushoto na Naibu Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Mwigulu Nchemba wakimnadi mgombea Ubunge wa Jimbo la Kalenga kupitia chama hicho cha CCM,Ndugu Godfreya Mgimwa,kwenye mkutano wa hadhara wa kampeni za lala salama,uliofanyika leo jioni katika kijiji cha Magulilwa kata ya Magulilwa,Iringa vijijini.
Kinana amewataka wakazi wa Kalenga kumpigia kura za kutosha na hatimae kuibuka mshindi kwa maendeleo ya jimbo hilo,hapo siku ya jumapili ambapo uchaguzi utanfanyika.Uchaguzi unafanyika ndani ya jimbo hilo kuziba nafasi ya aliyekuwaMbunge wajimbo hilo kwa tiketi ya CCM,Marehemu William Mgimwa.
Katibu Mkuu wa CCm,Ndugu Kinana akiwahutubia wakazi wa kijiji cha Magulilwa mapema leo jioni wakati wa mkutano wa kampeni za lala salama,alipokuwa akimnadi mgombea Ubunge kupitia chama hicho,Ndugu Godfreya Mgimwa kwa wananchi.
Mgombea Ubunge Jimbo la Kalenga kwa tiketi ya CCM,Ndugu Godfreya Mgimwa akijinadi kwa wakazi wa kijiji cha Magulilwa,kata ya Magulilwa Iringa Vijijini wakati wa mkutano wa kampeni za lala salama,amapo uchaguzi unatarajiwa kufanyika Machi 16,siku ya jumapili.
Naibu Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Mwigulu Nchemba akimnadi mgombea Ubunge wa Jimbo la Kalenga kupitia chama hicho cha CCM,Ndugu Godfreya Mgimwa,kwenye mkutano wa hadhara wa kampeni za lala salama,uliofanyika leo jioni katika kijiji cha Magulilwa kata ya Magulilwa,Iringa vijijini.
Wananchi wa kijiji cha Magulilwa wakishangilia jambo.
Mmoja wa wakazi wa kijiji cha Magulilwa akisoma moja ya gazeti la kila siku wakati mkutano wa hadhara wa kampeni za uchaguzi,ukiendelea jioni ya leo.
Mbunge wa jimbo la Ludewa,Mh.Deo Filikunjombe akiagana na Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana mara baada ya kumlaiza mkutano wa hadhara wa Kampeni,kwa ajili ya kumnadi mgombea wa CCM jimbo la Kalenga,Ndugu Godfrey Mgimwa,uliofanyika jioni ya leo kwenye kijiji cha Magulilwa,Iringa vijijini,pichani kati ni Mbunge wa jimbo la Mwibala,Mh Kangi Lugora akisikiliza.PICHA ZAIDI BOFYA MICHUZIJR BLOG
Kaka Michuzi ujue unaheshima kubwa lakini nasikitika umekuwa kama TBC hutaki kutoa taarifa za mkutano ya yule mama wa CHADEMA, siyo siri nilidhani chombo chako ni cha jamii kama ITV. Nalazimika kuichukia blog yako ambayo nimekuwa nao toka unaanza. Shame on you brother, mambo ya kizamani sana hayo kaka.
ReplyDelete