Na Francis Godwin Blog
WANANCHI
wa Ludewa mkoani Njombe wamempongeza Rais Dr Jakaya Kikwete kwa
hatua yake ya kuwashirikisha wananchi wa maeneo husika katika suala
la utatuzi wa mgogoro wa mpaka kati ya Tanzania na Malawi
Hatua
ya wananchi hao kumpongeza Rais Dr Kikwete imekuja huku ikiwa
ni siku tatu zimepita toka mbunge wao wa jimbo la Ludewa Deo
Filikunjombe ,mbunge wa jimbo la Kyela Dk.
Harrison Mwakyembe na mbunge wa jimbo la Mbinga Magharibi John
Komba kurejea nchini kutoka Malawi katika kikao cha usuluhishi wa
mgogoro wa mpaka kati ya Malawi na Tanzania
Wakizungumza
na mwandishi wa habari hizi wananchi hao akiwemo Yohana Haule
walisema kuwa hatua ya Rais Kikwete kutumia wananchi wenye
kushughulikia suala hilo ni hatua ya kupongezwa kwani wabunge hao
ni wawakilishi wa wananchi hivyo kila kinachoendelea kitawafikia
mapema wananchi wa maeneo ya mpakani Malawi na Tanzania.
Haule
alisema kuwa imani na matumani ya wana Ludewa ni kuona mbunge wao
amewawakilisha katika suala hilo na kuwa hawana shaka na
uwakilishi wake na wanaamini watapewa mrejesho wa kila
kinachoendelea katika suala hilo.
Hivyo
alisema kwa sasa hofu ambayo awali wananchi wa
kando ya ziwa Nyasa walikuwa nayo juu ya mgogoro huo wa mpaka kati
ya Tanzania na Malawi imeanza kutoweka kutokana na mbunge wao
Filikunjombe kuzunguka maeneo yote ya Mwambao na kufanya mikutano na
kuwaondoa hofu juu ya hilo.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...