Rais wa Tanzania Red Cross, Dr. George
Nangale, akifurahia jambo wakati
akipokea mfano wa hundi ya Shilingi Milioni kumi kutoka kwa Mkuu wa kitengo cha kusaidia jamii"
Vodacom Foundation" Yessaya Mwakifulefule. Fedha hizo zimetolewa kwa chama
hicho kwa ajili ya kuimarisha huduma na kusaidia waliokumbwa na maafa ya
mafuriko yaliyotokea Wilayani Kilosa Mkoani Morogoro na kuacha mamia ya kaya
bila makazi. Wanaoshuhudia ni Mkurugenzi wa Maendeleo wa Chama cha Msalaba
Mwekundu, Julius Kejo na Meneja Uhusiano wa Nje wa Vodacom Tanzania,Salum
Mwalimu.
Rais wa Tanzania Red Cross, Dr. George Nangale, akisisitiza jambo kwa
waandishi wa Habari
(Hawapo pichani) punde baada ya kupokea msaada wa fedha, kiasi cha
Shilingi milioni
kumi kilichotolewa na Vodacom Tanzania kupitia kitengo chake cha
kusaidia jamii"Vodacom Foundation" kwa ajili ya kuimalisha
huduma na kusaidia waliokumbwa na maafa ya mafuriko yaliyotokea Wilayani
Kilosa
Mkoani Morogoro. Pamoja nae katika picha kutoka Kushoto ni Mkuu wa
Vodacom Foundation, Yessaya Mwakifulefule na Meneja Uhusiano wa Nje wa
Vodacom
Tanzania, Salum Mwalim.
Rais wa Tanzania Red Cross, Dr. George Nangale na Mkuu
wa kitengo cha kusaidia jamii cha Vodacom Tanzanaia"Vodacom Foundation" Yessaya Mwakifulefule, wakimsikiliza mmoja wa
Maafisa wa Tanzania Red Cross punde baada ya kupokea msaada wa fedha kiasi
cha Shilingi milioni kumi Kilichotolewa na Vodacom Tanzania kupitia kitengo hicho kwa
ajili ya kuimalisha huduma na kusaidia waliokumbwa na maafa ya mafuriko
yaliyotokea Wilayani Kilosa Mkoani Morogoro
Mkuu wa Kitengo cha kusaidia jamii cha Vodacom Tanzania" Vodacom Foundation" Yessaya
Mwakifulefule akizungumza na waandishi
wa Habari (Hawapo pichani) punde baada ya kutoa msaada wa fedha kiasi cha
Shilingi milioni kumi Kilichotolewa na kitengo hicho"Vodacom Foundation"kwa ajili
ya kuimalisha huduma na kusaidia waliokumbwa na maafa ya mafuriko yaliyotokea Wilayani
Kilosa Mkoani Morogoro. Pamoja nao katika picha ni Rais wa Tanzania Red Cross,
Dr. George Nangale (katikati)Meneja Uhusiano wa Nje wa Vodacom Tanzania,
Salum Mwalim.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...