Na Pascal Mayalla
Umetolewa wito kwa Mabenki kote nchini, zaidi ya kuzihudumia jamii kwa huduma za kifedha, pia ziikumbuke jamii inayowazunguka kwa kutoa huduma nyingine za kijamii, kama kusaidia mashule, mahospitali na jamii mbali hitaji, zinazohudumiwa na benki hizo.
Wito huo, umetolewa na Mkurugenzi wa Benki ya CRDB Tawi la Lumumba, Bw. John Almasi, wakati wa maandimisho ya siku ya wanawake Duniani, ambapo menejimenti na wafanyakazi wa Benki ya CRDB Lumumba, walifanya huduma za kijamii kwa kuwatembelea wagonjwa wa wodi ya wazazi hospitali ya Mnazi Mmoja, ambapo waliwapelekea vifaa vya usafi, kuwagawia miche ya sabuni, na kugawa vyandarua kwa wagonjwa wote wa wodi hiyo ya wazazi.
Bw. Almasi amesema benki yake wameamua kusherehekea sikukuu ya wanawake kwa kuwakumbuka wanawake wazazi waliolazwa hospitali ya Mnazi Mmoja.
Kwa upande wake Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Mnazi Mmoja, Dr. Kwaw, aliishukuru CRDB Lumumba kwa misaada hiyo, na kusema yeye na wagonjwa wake wamefarijika sana!. Pia ametoa wito kwa taasisi nyingine kuiga mfano huo wa CRDB Lumumba kuhudumia wagonjwa na kusisitiza kuwa jukumu la kuwahudumia wagonjwa na wahitaji mbalimbali, lisiachwe kwa serikali tuu au wanandugu, liwe ni jukumu la jamii.
Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya CRDB, Saugata Bandyopadhyay mwenye suti, katika picha ya pamoja wafanyakazi na wateja wa benki ya CRDB, Tawi la Lumumba, Mkurugenzi huyo alipotembelea tawi hilo leo asubuhi
![]() |
Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya CRDB, Saugata Bandyopadhyay akizungumza na Mkurugenzi wa CRDB, Tawi la Lumumba, John Almasi, Mkurugenzi huyo alipotembelea tawi hilo leo asubuhi. |
Wateja Walifurahije?. Ilikuwa ni mwendo wa vinyaji baridi
Mkurungenzi wa CRDB Bank, Tawi la Lumumba, John Almasi, akishiriki zoezi la usafi katika Hospitali ya Mnazi Mmoja kuadhimisha Siku ya wanawake Duniani.
Mkurungenzi wa CRDB Bank, Tawi la Lumumba, John Almasi, akishiriki zoezi la usafi katika Hospitali ya Mnazi Mmoja kuadhimisha Siku ya wanawake Duniani. Kwa picha zaidi BOFYA HAPA
Leo umenifurahisha sana ankal kwa hicho kiswakinge ulianza na Deputy MD, halafu ukanipa Deputy Naibu Mkurugenzi Mkuu.
ReplyDelete