Mke wa Rais na Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo, WAMA, Mama Salma Kikwete akizindua rasmi upimaji wa saratani ya  mlango wa kizazi wakati wa kilele cha siku ya wanawake duniani katika sherehe iliyofanyika katika uwanja wa Nyamagana huko Mwanza
 Mke wa Rais Mama Salma Kikwete mara baada ya kuzindua rasmi upimaji wa saratani ya mlango wa kizazi aliwakabidhi Waganga wakuu wa mikoa ya Mwanza, Iringa, Mbeya na Mara vifaa  vya kupima saratani hiyo. Pichani Mama Salma Kikwete akimkabidhi Mganga Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Dkt. Valentino Bangi mkoba wenye vifaa vya upimaji.
  Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akisikiliza maelezo kutoka kwa Dkt. Nestory Masalu kutoka hospitali ya Rufaa ya Bugando ambaye alikuwa akiwapima akina mama katika kituo cha Afya cha Buzuruga kilichoko katika wilaya ya Ilemela mkoani Mwanza mara baada ya kuzindua rasmi upimaji wa saratani  ya mlango wa kizazi katika uwanja wa Nyamagana na kutembelea kituo hicho ambapo wanawake wengi walijitokeza kwa ajili ya kupima. Kwa picha zaidi BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...