Picha na Habari, John Nditi, Morogoro
LICHA ya madereva wa daladala wa Manispaa ya Morogoro kusitisha mgomo uliodumu saa 10 siku ya Jumatano , Machi 19, mwaka huu na kwa Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Morogoro , Faustine Shilogile, kusisitiza kuwa Askari wa Kikosi cha Usalama Barabarani wataendelea kuzikamata daladala zitakazovunja sheria , baadhi ya madereva na makonda wao wamekuwa ni vichwa sugu kwa ukiukwaji wa sheria hizo.
Dereva na konda wa daladala lenye namba za usajili T 870 AED linalofanya kazi za kusafirisha abiria Kihonda- Mjini kwa makusudi na kiburi cha hali ya juu wamemua kuweka kituo cha kupakia abiria barabarani kabisa karibu na Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Morogoro kwenye kona ya barabara ya zamani ya Dar es Salaam eneo lisiloruhusiwa na ni hatari kwa kuweza kusababisha ajali kwa watumiaji wengine kama inavyoonekana pichani.
Na huyu ni mmoja tu ya mifano hai ya ujeuri wa watu hawa. Kila mahali hali ni kama hii, na wakichukuliwa hatua huja juu na hata kugoma kutoa huduma.
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Morogoro, ACP Faustine Shilogole , akizungumza na waandishi wa habari jana tu, mjini hapa kuhusiana na mgomo huo alisema kuwa askari wa kikosi cha usalama barabarani wanafanya kazi zao za kukamata magari yanayokiuka sheria kwa mujibu wa sheria za usalama barabarani.
Kamanda huyo alisisitiza kuwa askari wa Usalama Barabarani hawapo kumwonea mtu , kazi yao ni kukamata magari mabovu na madereva wanaokiuka sheria za usalama barabarani na kupingwa faini kuligana na makosa yaliyojitokeza.
Ndiyo, hao daladala wamedekezwa na trafiki kwa uswahiba wa kinafiki. Trafiki wanacheka na kima na jamii inavuna mabua!
ReplyDeleteNi kweli maderva wa moro wana viburi sana. Wanapaki magari popote wanapotaka. Nenda pale ipoipo Mazimbu utawachukia kwa jinsi wanavyoziba njia za kwenye junctions.
ReplyDelete