Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisaini kitabu cha maombolezo ya msiba wa Lefoord Simba, mtoto wa Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Sophia Simba, wakati alipofika nyumbani kwa Waziri Masaki jijini Dar es Salaam, leo kutoa pole.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimfariji Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Sophia Simba, wakati alipofika nyumbani kwake Masaki jijini Dar es Salaam, leo kutoa pole kwa kufiwa na mtoto wake, Lefoord Simba. Mazishi yatafanyika kesho kwenye Makaburi ya Kinondoni.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Sophia Simba, wakati alipofika nyumbani kwa Waziri Masaki jijini Dar es Salaam, leo kutoa pole kwa kufiwa na mtoto wake, Lefoord Simba. Mazishi yatafanyika kesho kwenye Makaburi ya Kinondoni.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akijumuika na Rais Mstaafu wa awamu ya tatu, Benjamini Mkapa, Waziri mstaafu (wa pili kulia) Mjumbe wa Nec Wilaya ya Busega, Chegeni (kulia) na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Shinyanga, Khamis Mgeja, wakizungumza jambo wakati wakijumuika kwa pamoja katika maombolezo ya msiba wa Lefoord Simba, mtoto wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Sophia Simba, Masaki jijini Dar es Salaam, leo.
Baadhi ya waombolezaji.Picha na OMR

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...