Wafanyakazi Wanawake wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, wakiungana na wanawake wenzao kusherehekea siku ya Wanawake Duniani kwenye viwanja vya Mwembe Yanga Temeke jijini Dar es Salaam, Jumamosi Machi 8, 2014.
Lucy Raphael (Kulia), akifurahia jambo na wafanyakazi wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, baada ya kumtembelea na kumpatia zawadi kwenye hospitali ya Temeke jijini Dar es Salaam jana. Lucy ambaye amejifungua watoto mapacha ni miongoni mwa watu waliofaidika na zawadi mbalimbali zilizotolewa na Mfuko huo kwa hospitali hiyo.
Meneja wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, Kanda ya Temeke, Erica Sendegeya (Kushoto), akimvisha karatasi maalum (Pampers), mtoto huyu aliyelazwa kwenye hospitali ya Temeke jijini Dar es Salaam, Jumamosi Machi 8, 2014. Wafanyakazi Wanawake wa Mfuko huo, walitembelea hospitali hiyo jana Jumamosi ili kuwafariji na kuwapatia misada wagonjwa baada ya kushiriki sherehe za siku ya wanawake Duniani.
Wafanyakazi wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, wakigawa misada kwa wagonjwa kwenye hospitali ya Temeke jijini Dar es Salaam, Jumamosi Machi 8, 2014.
Meneja wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, Kanda ya Temeke jijini Dar es Salaam, Erica Sendegeya (Kushoto) na Mama wa Mapacha, Lucy Raphael (Kulia), wakifurahi, huku Erica akiwa amewabeba watoto hao, wakati Wafanyakazi Wanawake wa Mfuko huo, walipotembelea hospitali ya Wilaya ya Temeke jijini Dar es Salaam, Jumamosi Machi 8, 2014, ili kuwafariji na kuwapatia misada, baada ya wafanyakazi hao kushiriki matembezi ya kuadhimisha siku ya Wanawake Duniani kwenye viwanja vya Mwembeyanga.
Meneja Masoko na Uhusiano wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, Lulu Mengele (Kushoto), akiwa amempakata kichanga, saa chache baada ya kuzaliwa na kubahatika kukutana na wafanyakazi wanawake wa Mfuko huo waliotembelea hospitali ya Temeke kwa nia ya kuwafariji na kuwapatia misada mbalimbali Juammosi Machi 8, 2014. Ziara hiyo ni baada ya kushiriki matembezi ya maadhimisho ya siku ya Wanawake Duniani kwenye viwanja vya Mwembeyanga.
Meneja wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, Kanda ya Temeke jijini Dar es Salaam, Erica Sendegeye(Wapili kulia), akimpatia mama huyu mzazi, karatasi maalum za kujivunga watoto(Pampers), wakati wafanyakazi wanawake wa Mfuko huo, walipotembelea wagonjwa kwenye hospitali ya Temeke jana, ambako walitoa misaada mbalimbali ya vyakula na vifaa kuadhimisha siku ya Wanawake Duniani. Wakwanza kushoto ni Meneja Masoko na Uhusiano wa Mfuko huo, Lulu Mengele.
Afisa Masoko wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, akiwa amebeba boksi lenye maji ya Kilimanjaro akiingia nalo kwenye wodi, tayari kugawia wagonjwa
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...