Hajjat Amina Mrisho Saidi, 
Kamishna wa Sensa Tanzania 
Kuwapatia wanawake fursa katika nyanja zote ni muhimu kwa maendeleo ya kaya zao na hata taifa kwa ujumla. Kauli hiyo imejidhihirisha kwa Hajjat Amina Mrisho Saidi, Kamishna wa Sensa Tanzania mwaka 2012 ambaye baada ya kumaliza elimu ya msingi alijikita katika kuchunga mbuzi huko kwao mkoani Arusha akidhani ndoto ya elimu ya sekondari imetuwama! 
Hata hivyo jitihada za mama yake mzazi na zake yeye binafsi pamoja na serikali zilimwezesha kufika alipo sasa. Hajjat Amina alifunguka bayana katika mahojiano maalum na Assumpta Massoi wa Idhaa hii kuhusu siku ya wanawake duniani ambapo anaanza kwa kuelezea familia yao..
(KUSIKILIZA BOFYA HAPO CHINI)

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 5 mpaka sasa

  1. Swadaqta, Jazakulahu Hajjat Awla Amina,

    Jitihada zinahitajika saaana kuhakikisha Mabinti kwa wingi wanapata Elimu badala ya kuwakadiria kwa kuwaingiza ktk Ndoa za mapema za utotoni!!!

    ReplyDelete
  2. Kweli serikali ya Awamu ya Kwanza ilijali elimu bila kujali umasikini au utajiri wa mwanafunzi na familia yake.

    Miaka hii hali ni tofauti sijui Bunge la Katiba litasisitiza ELIMU na AFYA ni HAKI ya MSINGI bila kujali kama unauwezo wa kulipia au la.

    Mdau
    Mjamaa.

    ReplyDelete
  3. Salaam Hajat
    Swadakta. Maisha waliyoishi enzi hizoo wazazi wtu si ya leo. Tupeleke watoto wakike shule na kuhakikisha tunawafuatilia, tunawasikiliza na kuwapa kipaumbele. Sio kuwafanyisha kazi kama vibarua.

    ReplyDelete
  4. ndugu hajjat ktk sensa zote duniani zinazofanywa kipengele cha dini huwa ni sehemu kwani ni muhimu kujua masuala ya imani za watu ktk mipangilio ya nchi, lakini wewe ndugu yangu umesaliti waislamu na kuona kukiondoa kipengele hicho , hakika malipo yake utayakuta utapoingia kaburini na utapokutana na mola wako , na hutakuwa na msaidizi , kwa taarifa tu hija haifuti madhambi/dhuluma yote aliyofanya mtu kwa watu wengine , humfutia madhambi yale yanayohusiana yeye na mola wake ka vile sala , saumu na mengineyo, kwa hio hata uende hija kila mwaka haki za watu ulizozizuia zitakufuata mpaka kaburini, huenda ukawa umelipwa mamilioni mengi kwa hilo.

    ReplyDelete
  5. naunga mkono Amina kuwa kufanikiwa kielimu sio lazima wazazi wawe wasomi. mimi nina digrii 2 ktk fani ya afya lakimi lakini kufanikiwa kwangu ni jihudi ya mama yangu ambae hajasoma baba alikuwa msmi lakini hakuwa na msaada mkubwa kwangu kelimu na pia mimi mwenyew nilikuwa najitahidi. watoto wasiku hizi wanachangia kushusha kiwango cha elimu hawajitumi

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...