Makamu Mwenyekiti wa CCM-Bara,Ndugu Philip Mangula akiongea na Waandishi wa Habari
 Makamu Mwenyekiti wa CCM-Bara,Ndugu Phillip Mangula akiongea na Waandishi wa Habari kutoka vyombo mbalimbali mapema leo asubuhi ndani ya Ofisi za Makao makuu ya chama hicho,huku akiwaonesha picha iliyotumika kwenye moja ya gazeti la kila siku hapa nchini,kwamba baadhi ya Wapinzani wamekuwa wakitumia vibaya nafasi za kutafuta uongozi kwa kuwadhalilisha watoto kupitia umaskini wao walionao ikiwemo sambamba na watu wengine,jambo ambalo si haki na si sawa. 
 Makamu Mwenyekiti wa CCM-Bara,Ndugu Phillip Mangula akiongea na Waandishi wa Habari kutoka vyombo mbalimbali mapema leo asubuhi ndani ya Ofisi za CCM mkoa wa Iringa,mara baada ya kuwasili mkoani humo.Mangula amesema kuwa amekuja Iringa kuratibu na kuhakikisha kuwa chama chake kinamaliza kampeni zake za uchaguzi mdogo wa jimbo la Kalenga kwa utulivu na amani,akaongeza kuwa ingawaje wana taarifa ya baadhi ya watu wamejiandaa kufanya fujo,lakini kwa bahati nzuri wameyapata majina ya watu hao,"Majina hayo yako ishirini ntayataja hapo baadae ili wananchi kwa ujumla wajue taarifa hizo ambazo zinapaswa kupingwa na kulaaniwa kwa namna yoyote ile" alisema Mangula kwa msisitizo..
Pichani kati shoto ni Makamu Mwenyekiti wa CCM-Bara,Ndugu Phillip Mangula akipokelewa na Katibu wa CCM mkoa wa Iringa Mjini Ndugu,Hassani Mtenga na wanachama wengine,alipokuwa akiwasili kwenye Ofisi za CCM mkoa wa Iringa, mapema leo .PICHA NA MICHUZIJR-IRINGA.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...