)
Home
Unlabelled
Mh. Stephen Wasira na Mh. Augustino Lytonga Mrema wazungumzia Umuhimu wa Muungano
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Most read Swahili blog on earth
Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.
HOJA ZA MHESHIMIWA WASIRA KAELEZEA MBILI (1) TANGANYIKA NI KUBWA KULIKO ZANZIBAR, KWA MAANA HIYO GHARAMA YA MUUNGANO KAMA KUTAKUWA NI MUUNGANO WA SERIKALI TATU ITABEBWA NA TANYIKA.
ReplyDeleteHoja hii si imara. Jibu lake ni rahisi sana. Kuunganisha nchi ni utashi wa kisiasa, kama wananchi wake wanataka kutengeneza muungano waulizwe; kama hawataki basi. Kama kweli hatutumikii wakoloni wale basi hii hoja si ya msingi. Wananchi ndiyo wenye nchi. Gharama za mambo ya Muungano zitalipwa kulingana na pato la nchi husika. Kinachotakiwa kukubaliana ni asilimia ngapi ya pato ya nchi iwe ni kwa ajili ya kuchangia Muungano. Mfano ikikubaliwa asilimia tano ya pato la kila nchi ichangie kwenye kushughulikia mambo ya Muungano ndivyo iwe hivyo; kwa uwiano huo haijalishi kama nchi ni ndogo au ni kubwa. Kwa asilimia hiyo tano kama Tanganyika pato lake ni sh 1000 kwa mwaka, basi itachangia sh 50, na kama Zanzibar pato lake ni Sh. 100, itachangia sh 5. Kiasi cha asilimia cha uchangiaji kitakokotelewa kulingana na uwiano; ni hisabu ya mlinganyo rahisi tu inayotakiwa kufanywa.
Lingine ni kwamba udogo wa nchi si kigezo cha kuifanya nchi iwe tajiri. Kuna nchi nyingi duniani ambazo ni ndogo kuliko Tanzania lakini zina utajiri mkubwa kuliko Tanzania; mfano Singapore, Korea ya Kusini, Sweden, Hong Kong, Brunei, n.k. Kitu cha msingi ni siasa safi ya kumletea maendeleo yule anayeishi katika hilo eneo.
HOJA YAKE YA PILI NI KWAMBA MFUMO WA MUUNGANO ULIOPENDEKEZWA NA JAJI WARIOBA UTAFANYA SERIKALI YA MUUNGANO ISIWE NA UHUSIANO NA MWANANCHI KWA KUWA MAMBO MENGI YATAKAYOMHUSU MWANANCHI YATASHUGHULIKIWA NA NCHI HUSIKA.
Jibu: hoja hii si kubwa au siyo nzito. Kwanza tunatakiwa kufahamu kuwa kuna nchi mbili: Tanganyika na Zanzibar. Tanganyika ilipata uhuru wake mwaka 1961 toka kwa Waingereza na Zanzibar ilipata Uhuru wake mwaka 1963. Kila nchi inawajibu wa kutoa huduma itakayokidhi mahitaji ya wananchi wake. Kwa hiyo kuungana kwa nchi mbili tunategemea kuangalia maslahi ya kisiasa ya nchi husika. Maslahi ya kisiasa nikimaanisha kuleta tija kwa watu wake waliopo kwenye maeneo husika.Kwa hiyo mambo ambayo yanaonekana kuwa yanaweza kuboresha maisha ya wananchi wa pande mbili (Tanganyika na Zanzibar) ni ya kushirikiana na mengineyo yabaki chini ya nchi husika. Cha msingi kumsikiliza kila mshirika wa Muungano ni lipi anahitaji kushirikiana; kwa mtindo huo ndiyo tutajenga muungano imara. Vinginevyo tutaleta machafuko na nchi itaendelea kudidimia kwa uchumi.
Kila la kheri