Akizungumzia mkutano huo bwana Yusuph Kileo ambaye aliongoza timu ya maandalizi ya mkutano huo alibainisha hayo na kueleza mkutano huo umekamilika salama ambapo mambo mbalimbali yalipata kujadiliwa yahusuyo ulinzi mtandao “Cyber security” na kupigilia msumari kauli mbiu ya mwaka 2014 kua ni mwaka wa vitendo. 
Mwanzo wa mkutano bwana Craig Rosewarne (Mwenyekiti wa kundi linalojiuhisisha na maswala ya ulinzi mtandao (ISG) katika nchi za afrika ambaye pia ni Mkurugenzi mkuu wa kampuni Wolfpack inayo jihusisha na maswala ya ulinzi mtandao na mkurugenzi wa SANS ukanda wan nchi za Afrika na mashariki ya kati) alianisha hali ilivyo sasa na kusema kumekua na wimbi kubwa la makosa mtandao ambapo kila mwaka yanaongezeka kasi huku akitolea mifano mbali mbali ya matukio ya hivi karibuni. 
Aidha alipata kuanisha ukuaji wa teknologia ambapo inaendelea kukua kwa kasi na inavyo ongeza uwezekano wa kasi ya uhalifu mtandao kukua endapo jitihada za dhati hazitowekwa tayari ili kukabiliana na changamoto zinazo rudisha nyuma vita dhidi ya ulinzi mtandao. Akitolea mifano changamoto mbali mbalizinazopelekea ugumu katika ulinzi mtandao alianisha changamoto hizo ikiwa ni pamoja na:- 
1. Uhaba wa programu za kompyuta salama kimtandao huku akitolea mifano baadhi ya program za komputa zinavyo tengenezwa kutoa mwanya kwa wahalifu kupa urahisi kuingilia komputa za watumiaji wa program hizo 
2. Kutokuwepo na makubaliano ya pamoja ya kisheria katika mapambano dhidi ya makosa mtandao. 
3. Kutokuwa na ushirikiano wa kuunganisha nguvu kati ya serikali mbali mbali na sekta binafsi kutokomeza uhalifu huu ambao unaendelea kukua kwa kasi. 
4. Kutokua na elimu kwa jamii juu ya makosa mtandao na jinsi ya kukabiliana nayo katika ngazi ya ya mtu mmoja mmoja. 
5. Kutokuwepo na utayari kwa kuunda timu katka nchi mbali mbali zenye uwezo wa kukabiliana na uhalifu mtandao.
Kwa upande mwingine Bwana Martin Euchner kutoka ITU (International telecommunication union) wakala wa umoja wa mataifa inayoshughulikia maswala ya mawasiliano alianisha hatua mbali mbali mbali ambazo hadi sasa ITU imekua ikizichukua ili kujaribu kuunganisha nchi zote za umoja wa mataifa ili kwapamoja ziweze kupambana kupunguza uhalifu mtandao. 
Pia alipata kuzungumzia jitihada za dhati na mafanikio yaliyo patikana kupitia mpango wa COP (Child Online Protection) ambao umejikita kuhakiki watoto wanabaki salama mtandaoni, kauli iliyo ibua hoja nzito ya mchezo unao patikana kwenye simu hivi sasa ujulikanao kama “Talking angela” ambao umekua unachezwa na watoto wengi wadogo mtandaoni chezo ambao ume ukitiliwa shaka unaweza kuwa unatumika vibaya na wahalifu mtandao ili kukusanya sauti za watoto na picha zao zinazoweza kutumiwa vibaya baadae. 
Aidha bwana Eucner, aliweza kuzungumzia mpango kabambe ambapo mapitio na kuangalia kwa karibu changamoto mtandao katika nchi mbali mbali katika mwaka huu wa 2014 zinategemewa kufanyika katika nchi takriban 16 Tanzania ikiwa ni miongoni mwa nchi zitakazo weza kufaidika na mpongo huo.
 Kwa upande wa bwana Kileo, Aliweza kufafanua kwa kina uhaba mkubwa wa wataalam wa maswala mtandao katika ngazi ya kidunia kwa sasa na mahitajio ya wataalam imekua ni kubwa huku akitolea mfano katika nchi zilizo endelea kuwa na mikakati kabambe ya kuunda jeshi Mtandao ili kukabiliana na vita mtandao maarufu kama “Cyber war”. 
Bw. Kileo aliasa washiriki kuendelea kufahamu yakua swala la mitandao ni swala lisilo na mipaka ya kijografia na linaweza kufanywa na mhalifu kutokea maeneo yoyote bila kujali anadhuru nchi gani hivyo nguvu ya pamoja ni muhimu sana ili kuweza kukabiliana na hali mbaya iliyo sasa.
 Picha Ya pamoja ya waandalizi wa mkutano wa maswala ya ulinzi mtandao wakiwa katika mapunziko ya chakula cha mchana kabla ya kuendelea katika sehemu ya pili ya mkutano huo.
Baadhi ya wadau wakifuatilia mkutano huo ambapo ulipigilia msumari kauli mbiu iliyoainisha Mwaka 2014 uwe ni mwaka wa vitendo.
Yusuph kileo (kati) akiwa pamoja na Bwana Craig Rosewarne (kushoto) na Martin Euchner kabla ya kuelekea ukumbi wa mkutano

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. Kazı nzuri sana

    ReplyDelete
  2. Watanzania sasa wanakuja kwa kasi katika maswala haya ya ulinzi mtandao.
    Najivunia kuwa mbongo.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...