-Katika kusherehekea siku ya Wanawake Jumamosi hii tarehe 08-03-2014 Bendi yako PENDWA ya Twanga Pepeta ikishirikiana na Mdau wake mkubwa Christer Bella Mwingira na Rukia Saloon, kwa pamoja wameandaa bonge la Pati kwa ajili ya kusherehekea sikukuu hii.
Kwa mujibu wa Mkurugenzi wa ASET Asha Baraka (pichani), mnuso huo unataraji kufanyika ndani ya Twanga City Mango Garden ambapo muonekano wake utakuwa tofauti na siku za kawaida kwa kuwa ukumbi utapambwa vilivyo.
Amesema Mavazi rasmi yatakuwa ni ya ya rangi NYEKUNDU, NYEUPE na NYEUSI, na kwamba -Zawadi kedekede zitatolewa na Rukia Saloon na Christer Bella Mwingira kama vitenge na Khanga ambayo ni mavazi rasmi ya mwanamke.
Ameongezea pia kutakuwa na ofa maalum kwa ajili ya akina mama toka kwa Mkurugenzi wetu Asha Baraka kwa kila atakayefika katika onyesho atalipia Tshs 5,000. kuanzia saa mbili mpaka saa nne usiku.
-Kiingilio kitakuwa ni Tshs 10,000. kwa VIP
pamoja na kinywaji na kawaida ni Tshs 7,000/=
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...