Baadhi ya akinamama na watoto ambao kaya zao ziko kwenye Mpango wa kunusuru kaya masikini unaoratibiwa na TASAF wakisubiri huduma ya kliniki katika hospitali ya Manyamanyama wilayani Bunda mkoani Mara.
Baadhi ya wanawake wajawazito ambao kaya zao ziko katika mpango wa knusuru kaya masikini unaoratibiwa na TASAF wakiwa katika msitari wa kusubiri kuonana na Daktari katika hospitali ya Manyamanyama wilayani Bunda mkoani Mara.
Mratibu wa TASAF wilayani Bunda Nyasegwa Piloty akizungumza na akinamama walioko kwenye Mpango wa kunusuru kaya masikini kwenye zahanati ya Mcharo katika wilaya ya Bunda mkoani Mara.
Muuguzi wa hospitali ya Manyamanyama wilayani Bunda akitoa mafunzo kwa akinamama walioko kwenye Mpango wa kunusuru kaya masikini unaoratibiwa na TASAF waliohudhuria kliniki
Baadhi ya wanawake wajawazito ambao kaya zao ziko katika Mpango wa kunusuru kaya masikini unaoratbiwa na TASAF wakiwa katika hospitali ya Manyamanyama wilayani Bunda kuhudhuria kliniki ambalo ni moja ya masharti ya Mpango huo
===== ===== ======
Mpango wa kunusuru Kaya Masikini na zinazoishi kwenye mazingira hatarishi unaoratibiwa na Mfuko wa Maendeleo ya Jamii TASAF umewahamasisha akinamama wajawazito na wale wenye watoto wa chini ya miaka MITANO kuhudhuria kiliniki ili kulinda afya ya mama na mtoto.
Mratibu wa TASAF katika wilaya ya BUNDA bwana Nyasegwa Piloty amwaambia Waandishi wa habari waliotembelea zahanati ya Mcharo na Hospitali ya Manyamanyama kuwa mahudhurio ya akinamama wajawazito na watoto katika huduma za kliniki yameongezeka tangu kuanza kwa mpango wa kunusuru kaya masikini wilayani humo.
Naye Muuguzi katika hospitali ya Manyamanyama Beatrice Ludala amesema kuwa mwitikio wa akinamama wajawazito na watoto walioko kwenye kaya zilizoko kwenye mpango wa kunuru kaya masikini chini ya TASAF ni wa kuridhisha ikilinganishwa na hali ilivyokuwa miaka ya nyuma.
Mahudhurio ya mama mojamzito na watoto wenye umri wa chini ya miaka Mitano ni moja ya masharti muhimu ya kaya zilizoingizwa kwenye mpango wa kunusuru kaya masikini ili ziweze kuhudumiwa na mpango huo ulioanzishwa na serikali kupitia Mfuko wa Maendeleo ya Jamii nchini TASAF ambao unatakelezwa kwa awamu nchini kote.
Picha zifuatazo zinaonyesha akinamama na watoto wao wakiwa katika zahanati ya Mcharo na hosipitali ya Manyamanyama katika wilaya ya Bunda mkoani Mara.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...