Mkurugenzi wa Wanafunzi wanaochukua Mafunzo ya Shahada ya
kwanza katika Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE), Dk. Esther Mbise akimkaribisha
mgeni rasmi, Meneja Kiongozi
Uhusiano wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii ( NSSF), Eunice Chiume (katikati),wakati wa Semina kwa wanafunzi wa Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE), iliyofanyika katika chuoni hapo jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mkuu
wa Idara ya Masoko chuoni hapo, Felix Chale. Jumla ya wanachuo 180 walihudhuria semina hiyo.
Meneja Kiongozi Uhusiano wa NSSF, Eunice Chiume akitoa mada wakati wa semina ya kuwawezesha wanafunzi wa vyuo vya Elimu ya Juu kuwa na uelewa kuhusu Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF), pindi watakapomaliza elimu yao.
Baadhi ya wanafunzi wakimsikiliza kwa makini, Meneja Kiongozi Uhusiano wa NSSF, Eunice Chiume wakati akitoa mada katika semina hiyo.
Meneja Kiongozi Uhusiano wa NSSF, Eunice Chiume akitoa mada kuhusu faida za kuwa mwanachama wa NSSF.
Tunasikiliza kwa makini.
Baadhi ya maofisa wa NSSF wakigawa vipeperushi vyenye maelezo ya muhimu kuhusu NSSF.
Ofisa Uhusiano wa NSSF, Maife Kapinga akigawa vipeperushi kwa wanafunzi wa CBE wakati wa semina hiyo.
Tunajifunza hifadhi ya jamii.
Baadhi ya wanafunzi wa Chuo cha CBE wakisikiliza kwa makini kazi za mfuko wa hifadhi ya jamii na faida zake
Meneja Kiongozi Uhusiano wa NSSF, Eunice Chiume akijibu maswali ya wanafunzi wa CBE kuhusiana na mfuko wa Taifa Hifadhi ya Jamii wa NSSF.
Jonas Pera akiuliza swali.
Mwanachuo wa CBE, Hadson Mwakilima akiuliza swali kuhusu mafao ya NSSF.
Mwanafunzi aliyejitambulisha kwa jina la Mohamed akiuliza swali.
Wanafunzi wakipewa zawadi za fulana za NSSF.
Ofisa Uhusiano wa NSSF, Maife Kapinga akigawa zawadi ya Kalenda za NSSF kwa wanafunzi wa CBE.
Ofisa Uhusiano wa NSSF, Said Mohamed akifafanua jambo wakati wa semina hiyo.
Na Mwandishi Wetu
Ofisa Uhusiano wa NSSF, Said Mohamed akifafanua jambo wakati wa semina hiyo.
Na Mwandishi Wetu
WANAFUNZI wa Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE), wameaswa kujiunga na Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) ili wanufaike na
mafao ya muda mrefu na ya muda mfupi yanayotolewa.
Hayo yalisemwa na Meneja Kiongozi wa NSSF, Eunice Chiume, kwenye semina na wanafunzi wa chuo hicho.
Aidha, katika semina hiyo, Eunice alianisha aina
za mafao yanayotolewa na Mfuko huo, ambayo ni ya miuda mrefu na mfupi.
Mafao ya muda mrefu alisema ni pamoja na
pensheni ya uzeeni, kuumia kazini na fao la mazishi, ambapo alisisitiza kuwa
fao la pensheni ya uzeeni ni muhimu zaidi kwa wanafunzi hao kwa kuwa
watanufaika na fao hilo watakapostaafu kazi.
Aidha, Eunice aliendelea kufafanua kwa fao
la pensheni ya ulemavu mfanyakazi hulipwa
kiinua mgongo endapo ataumia akiwa kazini na pensheni ya urithi endapo
kama unachangia mfuko wa NSSF ni vema akawajuza wanafamilia ili akifariki dunia
warithi wa marehemu wanufaike na penshen ya urithi.
Kwa upande wa mafao ya muda mfupi, Meneja Kiongozi
huyo aliyataja kuwa ni pamoja na matibabu, kuumia kazini na msaada wa mazishi.
Kwa
upande wa matibabu alisema NSSF hutoa matibabu bure kwa mke/mume na watoto wanne kama wana miaka 18
na miaka 21 kama bado wanasoma, ambapo alifafanua kuwa watapata matibabu bure
bila gharama za ziada kwa wanachama wake.
Meneja kiungozi huyo pia aliwaambia sasa
shirika limekuja na huduma mpya tatu ambazo zinalenga kuwanufaisha wanachama
wengi zaidi na mafao hayo ya NSSF. Huduma
hizo ni Hiyari , Mikopo ya riba nafuu na Westadi, ambapo zote alizitolea
ufafanuzi.
Aidha, kwa upande wake Mkurugenzi wa
wanafunzi wanaochukua shahada ya kwanza, Dk. Esther Mbise, alisema kuwa
semina hiyo ni nzuri kwa vijana wengi
kujua kuhusu huduma na kazi za
mifuko ya jamii.
Semina hiyo iliudhriwa na wanafunzi 180
wa CBE , wa mwaka wa tatu na wa pili, ikilenga kutoa elimu kwao ili wajue umuhimu
wa mifuko mara tu watakapoanza kujitegemea.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...