Mwenyekiti wa CCM shina la Essex Uingereza, Bibi Maryam Seif akigawa misaada hiyo kwa  watoto hao yatima wa  kituo cha Kurasin jijini 
Dar es salaam
 Bibi Maryam Seif, akiendelea kugawa misaada kwa watoto hao yatima wa Kurasini.
  Mwenyekiti wa CCM shina la Essex Uingereza, Bibi Maryam Seif,  akimkabidhi misaada hiyo mlezi wa  watoto hao yatima wa  kituo cha Kurasin jijini Dar es salaam
Bibi Maryam Seif, akiwa na baadhi ya watoto hao yatima wa Kurasini.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 8 mpaka sasa

  1. CCM Uingereza tawi la Essex mko juju na mimi binafsi nalikubali shina hili hasa Mwenyekiti wake. Bi Maryam nimekukubali Kama ni mpiganaji. Mfano huu uigwe na mashina mengine hapa hasa shina langu la Reading.

    ReplyDelete
  2. CCM inatisha jamani.. Mtake msitake hiki ni chama pekee ambacho hakina ubaguzi wa kijinsia rangi wala udini.. Dispora muige mfano si maneno mengi tu.. Vitendo ndio vinakupeleka peponi au motoni si maneno..

    ReplyDelete
  3. Hongera sana Bibi Maryam. Unastahili pongezi kwa juhudi uliyofanya kusafiri toka Uingereza na kuja Tanzania kusaidia yatima. Ni jambo la kheri na la kuigwa.
    Alhaj Suleiman

    ReplyDelete
  4. zeyana- katibu wa essexMarch 09, 2014

    shina la essex tunajivunia kwa upendo na umoja.

    ReplyDelete
  5. zeyana- katibu wa essexMarch 09, 2014

    essex oyee

    ReplyDelete
  6. Hongera shina la Essex.

    ReplyDelete
  7. Huruma ni sifa muhimu na njema sana kwa kiongozi. Tunakushukuru sana mwenyekiti wetu kwa kuelekeza huruma zako nyambani. -Ami Tuni Essex UK

    ReplyDelete
  8. Hivi wewe mdau namba #2 vipi? Sasa diaspora waige, unamaanisha nini? Hao watu wa Essex si diaspora? Au mie sielewi maana ya diaspora?. Au kwa vile wamesema CCM Essex?! Kama uelewi si uombe msaada jamaa wa diasora wakusaidie kukufanulia?(maana unapenda vya urahisi). Haya hunaweza Kugoogle maana ya diaspora. Kwanza, kukujibu, watu kibao wanasaidia kwa miaka kibao hawataki kujitangaza kwani kufanya hivyo mnaanza kusema anataka kugombea uongozi fulani au anapenda sifa. Ukitoa kwa upendo hauna haja ya kujitangaza, malipo kwa Mungu. Sasa naelewa kwa nini watu maarufu na viongozi Bongo wanakwenda na waandishi wa habari kutoa misaada. Sababu ya watu kama nyie wanajua mtawahukumu kuwauliza wametoa misaada ghani? Pili, toka lini mtu anaye ombwa kitu analazimishwa kama mnavyolazimisha diaspora watoe misaada? Tatu, ndiyo maana ndugu zenu wakienda wengine hawarudi kwa sababu hamuwapendi kwa moyo bali mnapenda pesa, na si kila mtu mambo yanamwendea sawa kwa vile yuko nje'. Tupendane kwa moyo Watanzania.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...