JAN ELOFF AKITOLEWA NJE YA KITUO CHA POLISI OYSTERBAY JIJINI DAR ES SALAAM
JAN ELOFF AKIHOJIWA NDANI YA CHUMBA MAALUM KILICHOPO NDANI YA KITUO CHA POLISI OYSTERBAY
Yule mzungu aliyekuwa anatafutwa na Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam kwa kutuhuma za kuwatapeli wananchi kwa Euro feki hatimae amekamtwa akijaribu kununua gari kwa pesa bandia.
Habari za uhakika zilizotua mezani zilisema mzungu huyo ambae ni Raia wa Afrika Kusini amefahamika kwa jina la JAN ELOFF mkaazi wa maeneo ya Msasani, Jijini Dar.
Taarifa zilisema mzungu huyo ambae alikuwa anatuhumiwa kumpiga zaidi ya Euro hizo feki 700 mwandishi (jina kapuni) a DTV mwanzoni mwa mwezi wa Januari mwaka huu kisha kufungua mashtaka kituo cha polisi Oysterbay na kupatiwa kumbukumbu hii OB/RB/ 2972/14 (KUJIPATIA PESA KWA NJIA YA UDANGANYIFU), pamoja na kutoa Euro Feki.
Baada ya tukio hilo la kutapeliwa mwanahabari huyo Jeshi la Polisi lilitangaza msako mkali wa kumtafuta mzungu huyo ambae alikuwa akishirikiana na wadada wawili ambao ni raia wa Cameroon na Nigeria pamoja na mwanaume wa kitanzania ambao baada ya kukamatwa mwenzao wanaendelea kutafutwa usiku na mchana na tayari ameshawataja wenzake anaoshirikiana nao. Kufuatia kukamtwa kwa mzungu huyo wananchi wengi wamempongeza Kamanda Kova kwa kufanikisha zoezi hilo.
Hata hivyo Jeshi la Polisi Kinondoni limetoa rai kwa mtu yeyote ambae amewahi 'kupigwa' na mzungu huyo basi wafike haraka kituo cha polisi Oysterbay kwa ajili ya kumtambua mzungu huyo.
Habari na Kili Nyepesi
Mahera au mahela angalia hicho kichwa cha habari
ReplyDelete