Meneja wa Mradi wa Kusaka Vipaji Vya Uigizaji Tanzania (Tanzania Movie Talents) Bw Joshua Moshi akiongea na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wakutambulisha kampeni mpya ya kusaka Vipaji vya uigizaji kutoka kampuni ya Proin Promotions Limited mapema leo katika Ofisi za Proin Promotions Limited, Mikocheni, Mtaa wa Ursino, Pembeni ni Meneja Masoko wa Proin Promotions Limited Bw Evance Stephen.
Muigizaji wa Filamu za Kitanzania Single Mtambalike almaarufu Richie Richie ambae pia ni mmoja wa majaji katika Shindano la kusaka vipaji vya uigizaji lijulikanalo kama Tanzania Movie Talents lililopo chini ya Kampuni ya Proin Promotions Limited akiongelea jinsi washindi watakavyopatikana katika shindano hilo linalotarajia kuanza tarehe 1 Aprili 2014
Mwandishi wa habari kutoka kituo cha Runinga Cha Channel Ten, Bw Fredy Mwanjala akiuliza swali kwa Meneja Mradi wa Tanzania Movie Talents, Bw Joshua Moshi (hayupo pichani) kuhusiana na Shindano la kusaka vipaji vya uigizaji nchini
Meneja Masoko wa Proin Promotions Limited, Bw Evance Stephen (wa kwanza kushoto) akionyesha stika za TRA ambazo zinaonyesha Uhalali wa filamu za Proin Promotions lakini Pia Wateja watakaonunua Filamu kutoka Proin Promotions wanatakiwa kutuma namba zilizopo kwenye stika hizo za TRA kwaajili ya kuweza kujishindia zawadi mbalimbali kutoka Proin Promotions kama Vile TV za Samsung na deki zake
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...