Mtalii Jeanne Traska kutoka Ujerumani
Bi.Jeanne Traska kutoka Ujerumani na Muongoza Wageni Athumani Juma wakiwa katika Lango la Marangu pamoja na vifaa mbalimbali walivyokwama navyo katika kilele cha Mawenzi Mlimani Kilimanjaro mara baada ya kuokolewa.

Kikosi cha Uokoaji katika Hifadhi ya Taifa Kilimanjaro kimefanikiwa kumuokoa mtalii Bi. Jeanne Traska (32) kutoka Ujerumani pamoja na muongoza wageni Athuman Juma ambao jana walikwama katika kilele cha Mawenzi Mlimani Kilimanjaro. Kikosi cha Uokoaji cha TANAPA kiliweza kufika eneo la kilele cha Mawenzi na kwa kutumia mbinu za uokoaji za kisasa kabisa kiliweza kuwanasua majira ya kumi na moja jioni.


Licha ya hali mbaya ya hewa iliyotokana na mawingu mazito katika eneo hilo, Kikosi cha Uokoaji cha TANAPA kiliweza kukabiliana na hali hiyo na kuweza kuwanasua na kisha kuwapeleka katika kituo cha Horombo majira ya saa mbili usiku ambapo walichukuliwa na gari kupitia njia maalum ya uokoaji na kufika katika Lango Kuu la Marangu saa nne na nusu usiku.


Hali ya hewa ilisababisha helikopta maalum iliyoletwa kwa ajili ya zoezi la uokoaji kushindwa kufanya kazi kwa kuwa mawingu mazito hayakuwezesha marubani kuliona eneo la kilele kwa urahisi.


Hivi sasa mtalii huyo pamoja na muongoza wageni wake bado wapo chini ya uangalizi wa hifadhi kwa kushirikiana na Kampuni ya Nordic Tours iliyomleta mgeni huyo.


Aidha, kwa kuwa ni tukio lisilo la kawaida, uongozi wa hifadhi unaendelea kuchunguza sababu zilizowafanya kuchepuka njia na kuelekea kilele cha Mawenzi badala ya Kibo. Kwa kawaida Kilele cha Mawenzi huwa hakitumiwi na watalii isipokuwa kwa kujaza fomu maalum inayoonyesha kuwa mgeni amekubali kwa hiyari yake kupanda kilele hicho.


Imetolewa na Idara ya Mawasiliano

Hifadhi za Taifa Tanzania

23.03.2014

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 11 mpaka sasa

  1. God is good & l thanks you for this infomation offcourse we need infomation like this may Godbless you

    ReplyDelete
  2. Kwa tabia za wazungu sasa utasikia ndoa kati ya mtalii na muongozaji wake,kwa kigezo eti walikuwa wote katika shida

    ReplyDelete
  3. Baniani asema...Janja iko, bana.

    ReplyDelete
  4. Mbona hawaonekani kama walipotea?...
    Sasa hivi utasikia wameoana na kija wetu keshaondoka kmfuata bibie ulaya...

    ReplyDelete
  5. Itabidi huyo mzungu na huyo muongozaji wake washkishwe adabu ili iwe fundsho kwa wengne wenye kufanya michepuko bila kufuata utaratibu....

    ReplyDelete
  6. kuna ubaya gani

    ReplyDelete
  7. Mbona hamsemi kwanini hicho kilele cha Mawenzi huwa hakitumiki? Yaani hamuoni kama mnaacha swali muhimu bila kujibiwa??

    ReplyDelete
  8. mlitaka wakutwe mahututi ndio muamini walikwama jamani.!!!!!

    ReplyDelete
  9. Jambo la ajabu mbona haikutangazwa kuwa mtanzania naye kapotea? Hivi tuna kasumba gani hatujithamini tunathamini wageni? Angalia kukitokea ajali kama kuna waeurope au amerika huwa wanafuatilia watu wao sisi hatuthamini kabisa hata kutangaza!!!!!!

    ReplyDelete
  10. Mdau hapo juu angalia vizuri,sio kupotea,yaani hawakupotea au huyo mthungu hakupotea isipokuwa walikwama au alikwama.Pia kuthamini ilikuwepo au ipo la si hivyo kusingeliwekwa helikopta kwa kazi za ajali kama hizo na ndio maana kopta ilitumika kwenda kuwakwamua lakini kutokana visibility ya waokowaji wa kopta kuwa mbaya ndio maana ilishindwa.

    ReplyDelete
  11. na akishaenda ulaya atapewa uraia kwa mgongo wa mkewe...kisha atakuwa mwana diaspora na baadae ataanza kuchukiwa kama wanavyochukiwa wana diaspora wengine kwa sababu waliondoka kwenda kutafuta maisha nje...

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...