Mtalii Jeanne Traska kutoka Ujerumani
Bi.Jeanne Traska kutoka Ujerumani na Muongoza Wageni Athumani Juma wakiwa katika Lango la Marangu pamoja na vifaa mbalimbali walivyokwama navyo katika kilele cha Mawenzi Mlimani Kilimanjaro mara baada ya kuokolewa.
Kikosi cha Uokoaji katika Hifadhi ya Taifa Kilimanjaro kimefanikiwa kumuokoa mtalii Bi. Jeanne Traska (32) kutoka Ujerumani pamoja na muongoza wageni Athuman Juma ambao jana walikwama katika kilele cha Mawenzi Mlimani Kilimanjaro. Kikosi cha Uokoaji cha TANAPA kiliweza kufika eneo la kilele cha Mawenzi na kwa kutumia mbinu za uokoaji za kisasa kabisa kiliweza kuwanasua majira ya kumi na moja jioni.
.jpg)
Hali ya hewa ilisababisha helikopta
maalum iliyoletwa kwa ajili ya zoezi la uokoaji kushindwa kufanya kazi kwa kuwa
mawingu mazito hayakuwezesha marubani kuliona eneo la kilele kwa urahisi.
.jpg)
Aidha, kwa kuwa ni tukio lisilo la
kawaida, uongozi wa hifadhi unaendelea kuchunguza sababu zilizowafanya
kuchepuka njia na kuelekea kilele cha Mawenzi badala ya Kibo. Kwa kawaida
Kilele cha Mawenzi huwa hakitumiwi na watalii isipokuwa kwa kujaza fomu maalum
inayoonyesha kuwa mgeni amekubali kwa hiyari yake kupanda kilele hicho.
Imetolewa na
Idara ya Mawasiliano
Hifadhi za Taifa
Tanzania
23.03.2014
God is good & l thanks you for this infomation offcourse we need infomation like this may Godbless you
ReplyDeleteKwa tabia za wazungu sasa utasikia ndoa kati ya mtalii na muongozaji wake,kwa kigezo eti walikuwa wote katika shida
ReplyDeleteBaniani asema...Janja iko, bana.
ReplyDeleteMbona hawaonekani kama walipotea?...
ReplyDeleteSasa hivi utasikia wameoana na kija wetu keshaondoka kmfuata bibie ulaya...
Itabidi huyo mzungu na huyo muongozaji wake washkishwe adabu ili iwe fundsho kwa wengne wenye kufanya michepuko bila kufuata utaratibu....
ReplyDeletekuna ubaya gani
ReplyDeleteMbona hamsemi kwanini hicho kilele cha Mawenzi huwa hakitumiki? Yaani hamuoni kama mnaacha swali muhimu bila kujibiwa??
ReplyDeletemlitaka wakutwe mahututi ndio muamini walikwama jamani.!!!!!
ReplyDeleteJambo la ajabu mbona haikutangazwa kuwa mtanzania naye kapotea? Hivi tuna kasumba gani hatujithamini tunathamini wageni? Angalia kukitokea ajali kama kuna waeurope au amerika huwa wanafuatilia watu wao sisi hatuthamini kabisa hata kutangaza!!!!!!
ReplyDeleteMdau hapo juu angalia vizuri,sio kupotea,yaani hawakupotea au huyo mthungu hakupotea isipokuwa walikwama au alikwama.Pia kuthamini ilikuwepo au ipo la si hivyo kusingeliwekwa helikopta kwa kazi za ajali kama hizo na ndio maana kopta ilitumika kwenda kuwakwamua lakini kutokana visibility ya waokowaji wa kopta kuwa mbaya ndio maana ilishindwa.
ReplyDeletena akishaenda ulaya atapewa uraia kwa mgongo wa mkewe...kisha atakuwa mwana diaspora na baadae ataanza kuchukiwa kama wanavyochukiwa wana diaspora wengine kwa sababu waliondoka kwenda kutafuta maisha nje...
ReplyDelete