Mtafiti toka Taasisi ya Taifa ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu NIMR kituo cha Muhimbili Dkt. Godfather Kimaro akitoa wito kwa wanchi kujitokeza kwa aajili ya kupima afya zao mara tu wanapoona dalili za ugonjwa wa Kifua Kikuu ili kupunguza maambukizi mapya. Katikati ni Mkurugenzi wa NIMR kituo cha Muhimbili Dkt Godfrey Mfinanga na wa mwisho kulia ni Afisa habari Idara ya Habari MAELEZO Frank Mvungi.
Mkurugenzi wa Taasisi ya Taifa ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu NIMR kituo cha Muhimbili Dkt Godfrey Mfinanga akiwaeleza waandishi wa habari kuhusu hali ya maambukizi ya ugonjwa wa kifua kikuu , wa mwisho kulia ni Afisa habari Idara ya Habari MAELEZO Frank Mvungi. Picha zote na Georgina Misama-MAELEZO
Frank Mvungi-Maelezo
Serikali yaendelea kuimarisha Tafiti za kifua kikuu hapa nchini kwa kushirikiana na Taasisi za Kimataifa. Hayo yamesemwa na Mkurugenzi wa Taasisi ya Taifa ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu (NIMR) kituo cha Muhimbili Dkt.Godfrey Mfinanga wakati wa mkutano na waandishi wa Habari leo jijini Dar es salaam.
Akieleza Dkt.Mfinanga alisema kuwa NIMR kituo cha Muhimbili imefanikiwa kwa kiasi kikubwa katika tafiti kwa kushirikiana na Taasisi za kimataifa kama African Research Consortium for Ecosystem and Population Health (AFRIQUE ONE CONSORTIUM) na East African Consortium for Clinical Research ( EACCR).
Dkt Mfinanga alibainisha kuwa wastani wa wagonjwa 295 kati ya watu 100,000 hugundulika kuwa na TB ,ambapo Tanzania bara ilionekana kuwa na wagonjwa wengi zaidi kuliko Tanzania Visiwani,Vijijini kuliko mijini,watu wazima kuliko vijana,ambapo utafiti huo uko hatua za mwisho.
Akifafanua zaidi amesema tafiti zimeonyesha kuwa kwa wastani wa asilimia 35 ya wagonjwa wa TB huchelewa kugundulika kutokana na uelewa mdogo na tabia ya wananchi walio wengi kuchelewa kwenda Hosipitali. Dkt Mfinanga alitaja maeneo yanayoathiriwa na Ugonjwa wa kifua kikuu kuwa ni mapafu ,tezi,tumbo,figo, na hata ubongo ikiwa mgonjwa hatapata matibabu kwa wakati muafaka.
Katika hatua nyingine Dkt Mfinanga amesema kuwa NIMR kituo cha Muhimbili imefanya utafiti ambao umethibitisha kuwa kuna umuhimu wa kushirikisha jamii katika kusimamia matibabu ya wagonjwa wa TB (Community DOT-PCT).
Kufuatia utafiti huo Serikali ilianzisha mfumo huo ambao umeonyesha mafanikio makubwa kwa kuwa mgonjwa anachagua mahali pa kumezea dawa za TB kati ya nyumbani akisimamiwa na ndugu au kwenye kituo cha tiba akisimamiwa na mtoa huduma wa afya.
Naye mtafiti toka NIMR kituo cha Muhimbili Dkt. Godfather Kimaro alitoa wito kwa wananchi kuwahi hosipitali pale wanapoona dalili za ugonjwa wa Tb ambazo baadhi yake ni kikohozi kwa muda wa wiki mbili,homa za mara kwa mara na kukonda.
Kituo cha Utafiti cha Muhimbili (NIMR Muhimbili Centre) ni moja ya vituo nane vya Taasisi ya utafiti wa magonjwa ya Binadamu (NIMR) Kituo cha Muhimbili kilirithiwa kutoka lililokuwa Baraza la Afrika ya Mashariki mwaka 1980 wakati Taasisi ya Taifa ya Utafiti wa magonjwa ya Binadamu ilipoanzaishwa kwa sheria ya Bunge Namba 23 ya mwaka 1979.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...