Mheshimiwa michuzi
tunashukulu sana kwa kazi yako ya kutujulisha yanayoendelea TANZANIA leo
naomba unipe nafasi niweke ya moyoni mwangu na maoni yangu kuhusu huu
mstakabali wa kupata katiba ya Jamuhuri ya muungano wa Tanzania, mengi
yamekuwa yakisemwa sana kuhusu hii katiba au ni muundo ghani wa muungano
tunaoutaka,watu wengi na wana siasa wamesahu kwamba muungano huu na
katiba hii ya zamani ndio umetufanya tuwe na undungu na pia tuwe na
amani mpaka hapa tulipo watu wengine wameandika katiba baada ya kumwaga
damu na nitatowa mfano Kenya,Rwanda,Uganda,Burundi na majirani zetu wa
Congo je hawa wana siasa wa CCM,CUF,CHADEMA haya yote mnaonekana kwenye
macho yenu na kwenye masikio yenu hamkuyaona au kuyasikia,
Wazee wetu waliotangulia walikuwa na nia nzuri sana lakini leo
inaonekana ndoto zao zitakufa na muungano wetu ambao umetupa amani na
maendeleo yetu tuliyonayo mpaka leo yako mashakani,na hii ni kutokana na
watu wanaosema wanawalilia waTanzania kumbe ni ni watu walio na agenda
ambazo nizawakutumikia vibaraka wa nje ,
IT IS TIME, WE ARE TIRED OF YOUR NOISE, IT TIME YOU NEED TO WORK .
Israel
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...