Benki ya NMB kwa kushirikiana na kampuni tatu yaani Fair Deal Auto Private Ltd inayosambaza pikipiki za miguu miwili na mitatu aina ya Bajaji, kampuni ya Car & General Limited Ltd inayosambaza pikipiki za miguu mitatu aina ya TV’S King pamoja na kampuni ya Quality Motors inayosambaza pikipiki za miguu miwili aina ya Honda wameingia ubia ili kuwawezesha wananchi kupata mikopo nafuu ya kumiliki pikipiki za miguu miwili na mitatu.
Hii yote ni katika kuendeleza azma ya NMB inayolenga kubuni huduma na bidhaa mbali mbali za kibenki zinazogusa kwa karibu mahitaji ya wateja na watanzania kwa ujumla.
Akizungumza
katika hafla ya uzinduzi wa mikopo hii jijini Mwanza, Waziri wa Uwezeshaji na Uwekezaji
kutoka ofisi ya Waziri Mkuu, Mhe. Dkt. Mary Nagu amesema “Mikopo hii ya pikipiki itawasaidia sana
vijana na wananchi kwa ujumla kuweza kumiliki pikipiki zitakazowawezesha
kuendesha maisha yao ya kila siku.
"Binafsi natambua ajira kwa vijana imekua ni
changamoto maeneo mengi nchini hivyo basi ningependa kuwasisitiza vijana
wachukue fursa hii inayotolewa na NMB kuweza kumiliki biashara zao wenyewe na
kujikimu kiuchumi”, alisema.
Vilevile kutoka NMB, Mkuu wa Kitengo cha Biashara za kibenki,
Bw. Filbert Mponzi amesema kuwa bidhaa hii mpya ina lenga kupunguza
changamoto za ajira kwa vijana hapa nchini.
“NMB itaendelea
kubuni bidhaa ili kupambana na changamoto za ajira zinazowakumba wateja.
tutaendelea kushirikiana na makampuni kama Fair Deal Auto Private Ltd, Car &
General Limited Ltd pamoja na Quality Motors ili kupata bidhaa zenye ubora
zaidi.” alisema Mponzi.
Marejesho ya mkopo huu wa pikipiki ya miguu
miwili na mitatu yanatolewa ndani ya muda wa miezi 24, ambapo kwa kipindi hiki chote,
mteja ataendelea kurejesha makato yake ya kila mwezi kwa kuzingatia taratibu za
makubaliano yatakayofanyika baina ya mteja na benki ya NMB.
Mikopo hii pia inawekewa bima kwa ajili ya
ulemavu au kifo kitakachomtokea mmliki wa pikipiki iliyochukuliwa mkopo. Bima
hii ni kwa ajili ya kumpa unafuu mkopaji endapo atapata matatizo ya kiafya
ambayo yatamfanya apate ulemavu au kupoteza maisha.
Mikopo hii yenye masharti nafuu inatolewa kwa mteja yeyote ambaye
atatitimiza vigezo vilivyowekwa ili kupata mkopo huu. Anachotakiwa kufanya
mteja ni kulipia asilimia thelathini ( 30%) ya bei ya pikipiki ya miguu miwili au mitatu kama inavyouzwa na wasambazaji wa pikipiki
hizi za Fair Deal Auto Private Ltd , Car & General Ltd pamoja na Quality
Motors.
Kwa maelezo zaidi temembelea matawi ishirini na moja tu ya NMB nchi
nzima yanayotoa mikopo hii kama ifuatavyo:
*Mwanza -Buzuruga na Kenyata Road,
*Dar es Salaam-Tegeta, Magomeni, Mwenge, Mbezi
Beach, Temeke, Ilala, Mlimani City, Msasani na Airport
*Arusha-Clock Tower na Arusha Market
*Manyara-Babati na Katesh
*Dodoma
*Mbeya-Mwanjelwa, Mbalizi Road na
Usongwe
*Moshi-Nelson Mandela na Tanga-Madaraka
NMB BENKI YAKO
Waziri wa nchi
ofisi ya Waziri Mkuu uwekezaji na uwezeshwaji, Mhe. Dkt. Mary Nagu akipeana
mkono na Mkuu wa Mkoa wa Geita Saidi Magalula wakati wa uzinduzi huo.
Waziri wa nchi
ofisi ya Waziri Mkuu uwekezaji na uwezeshwaji, Mhe. Dkt. Mary Nagu akimpongeza
Mkuu wa Kitengo cha Biashara za benki ya NMB, Bw. Filbert Mponzi wakati wa
uzinduzi wa mpango wa uwezeshwaji kwa wateja wa NMB kupitia mikopo ya pikipiki za
miguu miwili na mitatu kutoka benki ya NMB. Kushoto ni Meneja wa NMB Kanda ya ziwa, Bw. Straton Chilongola.
Waziri wa nchi ofisi ya Waziri Mkuu uwekezaji na uwezeshwaji, Mhe. Dkt
Mary Nagu akikata utepe kama ishara ya ufunguzi rasmi wa uwezeshwaji kwa wateja
wa NMB kupitia mikopo ya pikipiki za miguu miwili na mitatu kutoka benki ya
NMB. Uzinduzi huo ulifanyika katika hoteli ya
Tilapia ya jijini Mwanza
Mikopo inayowezesha vijana ni mizuri ila vijana waendeshe vyombo hivi kwa makini.
ReplyDelete