Benki ya NMB kwa kushirikiana na kampuni tatu yaani Fair Deal Auto Private Ltd inayosambaza pikipiki za miguu miwili na mitatu aina ya Bajaji, kampuni ya Car & General Limited Ltd inayosambaza pikipiki za miguu mitatu aina ya TV’S King pamoja na kampuni ya Quality Motors inayosambaza pikipiki za miguu miwili aina ya Honda wameingia ubia ili kuwawezesha wananchi kupata mikopo nafuu ya kumiliki pikipiki za miguu miwili na mitatu. 
 Hii yote ni katika kuendeleza azma ya NMB inayolenga kubuni huduma na bidhaa mbali mbali za kibenki zinazogusa kwa karibu mahitaji ya wateja na watanzania kwa ujumla.
Akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa mikopo hii jijini Mwanza, Waziri wa Uwezeshaji na Uwekezaji kutoka ofisi ya Waziri Mkuu, Mhe. Dkt. Mary Nagu amesema “Mikopo hii ya pikipiki itawasaidia sana vijana na wananchi kwa ujumla kuweza kumiliki pikipiki zitakazowawezesha kuendesha maisha yao ya kila siku. 
"Binafsi natambua ajira kwa vijana imekua ni changamoto maeneo mengi nchini hivyo basi ningependa kuwasisitiza vijana wachukue fursa hii inayotolewa na NMB kuweza kumiliki biashara zao wenyewe na kujikimu kiuchumi”, alisema.
Vilevile kutoka NMB, Mkuu wa Kitengo cha Biashara za kibenki, Bw. Filbert Mponzi amesema kuwa bidhaa hii mpya ina lenga kupunguza changamoto za ajira kwa vijana hapa nchini.
“NMB itaendelea kubuni bidhaa ili kupambana na changamoto za ajira zinazowakumba wateja. tutaendelea kushirikiana na makampuni kama Fair Deal Auto Private Ltd, Car & General Limited Ltd pamoja na Quality Motors ili kupata bidhaa zenye ubora zaidi.” alisema Mponzi.
Marejesho ya mkopo huu wa pikipiki ya miguu miwili na mitatu yanatolewa ndani ya muda wa  miezi 24, ambapo kwa kipindi hiki chote, mteja ataendelea kurejesha makato yake ya kila mwezi kwa kuzingatia taratibu za makubaliano yatakayofanyika baina ya mteja na benki ya NMB. 
Mikopo hii pia inawekewa bima kwa ajili ya ulemavu au kifo kitakachomtokea mmliki wa pikipiki iliyochukuliwa mkopo. Bima hii ni kwa ajili ya kumpa unafuu mkopaji endapo atapata matatizo ya kiafya ambayo yatamfanya apate ulemavu au kupoteza maisha.

Mikopo hii yenye masharti nafuu inatolewa kwa mteja yeyote ambaye atatitimiza vigezo vilivyowekwa ili kupata mkopo huu. Anachotakiwa kufanya mteja ni kulipia asilimia thelathini ( 30%)  ya bei ya pikipiki ya miguu miwili  au mitatu  kama inavyouzwa na wasambazaji wa pikipiki hizi za Fair Deal Auto Private Ltd , Car & General Ltd pamoja na Quality Motors. 
Kwa maelezo zaidi temembelea matawi ishirini na moja tu ya NMB nchi nzima yanayotoa mikopo hii kama ifuatavyo: 
*Mwanza -Buzuruga na Kenyata Road,
*Dar es Salaam-Tegeta, Magomeni, Mwenge, Mbezi Beach, Temeke, Ilala, Mlimani City, Msasani na Airport
*Arusha-Clock Tower na Arusha Market
*Manyara-Babati na Katesh
*Dodoma
*Mbeya-Mwanjelwa, Mbalizi Road na Usongwe
*Moshi-Nelson Mandela na Tanga-Madaraka
                                                        NMB BENKI YAKO

Waziri wa nchi ofisi ya Waziri Mkuu uwekezaji na uwezeshwaji, Mhe. Dkt. Mary Nagu akipeana mkono na Mkuu wa Mkoa wa Geita Saidi Magalula wakati wa uzinduzi huo.
Waziri wa nchi ofisi ya Waziri Mkuu uwekezaji na uwezeshwaji, Mhe. Dkt. Mary Nagu akimpongeza Mkuu wa Kitengo cha Biashara za benki ya NMB, Bw. Filbert Mponzi wakati wa uzinduzi wa mpango wa uwezeshwaji kwa wateja wa NMB kupitia mikopo ya pikipiki za miguu miwili na mitatu kutoka benki ya NMB. Kushoto ni Meneja wa NMB Kanda ya ziwa, Bw. Straton Chilongola.
Waziri wa nchi ofisi ya Waziri Mkuu uwekezaji na uwezeshwaji, Mhe. Dkt Mary Nagu akikata utepe kama ishara ya ufunguzi rasmi wa uwezeshwaji kwa wateja wa NMB kupitia mikopo ya pikipiki za miguu miwili na mitatu kutoka benki ya NMB. Uzinduzi huo ulifanyika katika hoteli ya Tilapia ya jijini Mwanza

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Mikopo inayowezesha vijana ni mizuri ila vijana waendeshe vyombo hivi kwa makini.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...