Ofisa Uhusiano wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Maife Kapinga akimkaribisha Waziri wa Habari Vijana Utamaduni na Michezo, Dk. Fenella Mukangara wakati alipotembelea banda la NSSF wakati wa maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani iliyoambatana na bonanza la michezo lililofanyika DUCE jijini Dar es Salaam, mwishoni mwa wiki. NSSF walidhamini bonanza hilo.
Wachezaji wa timu ya
mpira wa kikapu ya Don Bosco wakipata maelezo kutoka kwa Maofisa Uhusiano wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Anna
Nguzo (kushoto), na Maife Kapinga kuhusu mafao yanayotolewa na shirika hilo,
wakati wa bonanza la michezo lililoandaliwa na Shirikisho la Mpira wa Kikapu
Tanzania (TBF), kwa ajili ya kusherehekea Siku ya Wanawake Duniani na
kudhaminiwa na NSSF.
Mshambuliaji wa timu ya mpira
wa Kikapu ya Wanawake ya Jeshi Stars, Jabu Shaban akimiliki mpira huku akizongwa
na mlinzi wa timu ya Don Bosco, Winnie Jogelea wakati wa Bonanza maalumu la
maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani ambalo liliandaliwa na Shirikisho la
Mpira wa Kikapu Tanzania (TBF), na kufanyika jijini Dar es salaam jana. Bonanza
hilo lilidhaminiwa na Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF).
Mchezaji wa timu ya mpira wa kikapu ya Jeshi Stars, Lucy Augustino (kushoto), akiifungia timu yake wakati wa mchezo wa bonanza lililoandaliwa na Shirikisho la mpira wa Kikapu Tanzania (TBF), na kudhaminiwa na Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Dunuiani.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...