Napenda kuwajulisha kwamba Semina ya Mawakala wanaoandaa mashindano ya urembo ya Redds Miss Tanzania 2014 inafanyika kesho tarehe 25 na 26 Machi 2014, katika ukumbi wa hotel ya Regency Park iliyopo Mikocheni jijini DSM. 
Semina hii ambayo itajumuisha Mawakala zaidi ya 70 kutoka Kanda, Wilaya, Vyuo na Mikoa yote ya Tanzania itawapa nafasi Mawakala kujadili Mafanikio na Changamoto za mashindano haya ambayo kwa mwaka huu yanatimiza miaka 20 tangu yaanzishwe mwaka 1994. 
Kwa mara nyingine tena Kampuni ya Swahili Media group kutoka Washington DC Marekani wamepewa kibali cha kuandaa mashindano haya kwa Watanzania wasichana wanaoishi nchini humo, ambapo mshindi wake ataungana na warembo wengine 30 watakao ingia Fainali za Taifa za mwaka huu ambazo zimepangwa kufanyika baadae mwezi wa Septemba. 
Pamoja na waraka huu nawatumia orodha Kamili ya Mawakala pamoja na mikoa wanayo wakilisha.
HIDAN  RICCO.
PRO, LINO INTERNATIONAL AGENCY.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...