Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Katiavi Afande Dhahiri Kidavashari akionesha meno ya tembo vipande 2 yenye thamani ya shilingi 22  aliyokamatwa nayo mtuhumiwa Bathoromeo Mtongwa Machi 8, 2014 katika kijiji cha Kilida, tarafa ya Mamba wilaya ya Mlele ambapo pia mtuhumiwa huyo alikamatwa na gobole 1 na risasi 14.
Mkaazi wa kijiji cha Kilida tarafa ya mamba wilaya ya mlele Bathoromeo Mtongwa (58) akiwa katika kituo cha polisi cha mkoa wa Katavi baada ya kukamatwa na meno mawili ya tembo yenye uzito wa kilo 15 yenye thamani ya shilingi milioni 22 na gobole moja pamoja na risasi 14. 
-------------------------
Na Walter Mguluchuma, 
Mpanda, Katavi
Mtu mmoja aliyefahamika kwa jina la Bathoromeo James Mtongwa mkaazi  wa Kijiji cha Kilinda Tarafa ya Mamba Wilaya ya Mlele Mkoa wa Katavi amekamatwa akiwa na vipande viwili vya meno ya tembo vyenye uzito wa kilo 15 vyenye thamani ya shilingi milioni 22 pamoja na bunduki moja aina ya Gobore na Risasi 14
Kwa mujibu wa Kamanda wa Jeshi la Polisi wa Mkoa wa Katavi Kamishna mwandamizi msaidizi  Dhahiri Kidavashari.  mtuhumiwa huyo alikamatwa Machi 7, mwaka huu majira ya saa mbili na nusu usiku.
Alisema mtuhumiwa alikamatwa kufuatia taarifa toka kwa raia wema ambazo ambazo zililifikia jeshi la polisi pamoja na askari wa Hifadhi ya Taifa ya Katavi kuwa mtuhumiwa anamiliki nyara za Serikali kinyume cha sheria.
Alifafanua  siku hiyo ya tukio majira ya saa mbili usiku polisi wakiwa na Askari wa Hifadhi ya Taifa ya Katavi walifika kwenye kijiji hicho cha Kilinda nyumbani kwa mtuhumiwa Bathoromeo na kufanya upekuzi nyumbani kwa mtuhumiwa na kufanikiwa kukamata risasi 14.
Kamanda Kidavashari alieleza wakati askari hao wakiendelea na upekuzi kwa kushirikiana na uongozi wa kijiji walilitilia shaka eneo moja la nyumba hiyo ya mtuhumiwa kutokana na eneo hilo kuonekana kuwa limechimbwa hivi karibuni.
Alisema  askari walipoamua kuchimba eneo hilo na baada ya kufukua kwa kitambo kidogo walifanikiwa kukuta meno ya Tembo vipande hivyo vya meno ya tembo vikiwa vimefukiwa ardhini hapo.
Baada ya kukamatwa kwa maneno hayo ya Tembo polisi walianza kumhoji mshitakiwa kwa kumtaka awaelekeze sehemu ambayo amekuwa akihifadhi Silaha ambayo amekuwa akiitumia kwenye matukio ya ujangili
Kamanda Kidavashari alieleza baada ya mahojiano mtuhumiwa aliweza kueleza kuwa bunduki ambayo amekuwa akiitumia kwenye matukio ya ujangili ameificha eneo linaloitwa King’anda lililopo ndani ya Hifadhi ya Taifa ya Katavi.
Alisema mnamo Mnamo Machi 8, 2014 majira ya saa nane mchana mtuhumiwa aliwaongoza Askari Polisi na Askari wa Hifadhi ya Taifa ya Katavi hadi eneo la King’anda  na kuwaonyesha silaha hiyo  kwenye kichaka.
Mtuhumiwa anatarajiwa kufikishwa Mahakamani wakati wowote mara baada ya upelelezi wa tukio hili utakapokamilika mapema iwezekanavyo.
Pia jeshi la polisi Mkoa wa Katavi lanatowa wito kwa wananchi kuendelea kutoa ushirikiano kwa jeshi la polisi kwa kutowa taarifa za watu wanaojihusisha na uwindaji haramu wa rasilimali za Taifa ili kulinda na kuhifadhi rasilimali zetu kwa manufaa ya vizazi vijavyo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 11 mpaka sasa

  1. HAHAHAHAHAHAHAHA....JAMAA ILO POZI LAKE.....KAYAKANYAGA....KIPINDI KIBAYA....HAHAHAHAHA

    ReplyDelete
  2. Tanzaniaaaaa Huyu ndie aliyeua tembo iliakauze meno nje ya nchi????

    ReplyDelete
  3. Khaaa..mmeanza sasa kukamata vidagaa na kutangaza kama vile ndo mnapambana wakati mapapa na wachina mnawaaacha...hivi hii nchi imerogwa na nani??its shame really!
    Mdau wa UK

    ReplyDelete
  4. ANAKULA POZI KWASABABU ANAJUA YEYE NI MASKINI TUU HANA LA KUPOTEZA MAPAPA WENYEWE WENYE BIASHARA HIYO HAWAKAMATWI!!

    ReplyDelete
  5. Alitumwa huyo na vigogo

    ReplyDelete
  6. mbona anatia huruma kweni hakujua AMA ZAKE AMA ZAO?

    ReplyDelete
  7. Muonekano tu inaonyesha huyo anatumiwa na wenye mtandao wa hiyo biashara na yeye anatafuta hela ya kula tu. Abanwe ili awataje wanaomtumia katika biashara hiyo vinginevyo ni kupiga risasi kichaka na kumuacha jangili pembeni.

    ReplyDelete
  8. Please mjue tofauti ya meno na pembe, meno huwa yanaota mdomoni na pembe ndio zile zinazochomoza nje. Hizo ni pembe za ndovu

    ReplyDelete
  9. Polisi kwa nini msi mbinye kibindoni awataje Mabosi wake waliomtuma?

    Yeye ni Zagalo tu ametumiwa !

    ReplyDelete
  10. Hahahaha!,

    Wadau jamani,

    Bathoromeo Mtongwa ametoa Pozi kali ktk Picha kwa kuwa ni siku nyingi sana akiwa kijijini hajapiga picha tokea mwaka 1978 akiwa Shule ya Sekondari Nkasi-Kantalamba wakati wa picha za black and white!

    Hivyo ameona aitumie hiyo nafasi adimu ya picha ya Polisi kwa kutoa Pozi lake maana alikuwa na kiu sana ya kupigwa picha !!!

    ReplyDelete
  11. Usoni Bathoromeo Mtongwa kama ndugu yake 'mtoto wa Mkulima Pinda' vile?

    Au duniani wawili wawili ni kwa kuwa ni mtu wa Mkoa wa Rukwa?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...