Meneja Masoko
na Elimu kwa Umma toka Mfuko
wa Taifa wa Bima ya Afya ( NHIF) Bi Anjela Mziray akiwaeleza waandishi
wa habari leo Jijini Dar es salaam kuhusu programu ya upimaji wa Afya kwa
wananchi kwa magonjwa yasiyoambukiza inayoendeshwa na mfuko huo hapa
nchini.kulia ni Meneja Uhakiki na Madai wa mfuko huo Dk.Clement Masanja na
kushoto ni Afisa habari ,Idara ya Habari Maelezo Bi Fatma Salum.
Meneja
Uhakiki na Madai wa mfuko huo Dk.Clement Masanja akiwaeleza waandishi wa habari
kuhusu umuhimu wa kufanya mazoezi ili kujikinga na magojwa yasiyoambukiza kama
kisukari, msongo wa mawazo na shinikizo
la damu,kushoto ni Meneja Masoko na Elimu kwa Umma Bi Anjela Mziray
Baadhi ya
waandishi wa habari wakifuatilia mkutano wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya
(NHIF) uliofanyika leo jijini Dar es salaam uliolenga kuelimisha wananchi
kuhusu mapambano dhidi ya magonjwa yasiyoambukiza kama Kisukari,shinikizo la
damu na Saratani.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...